kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Tuwe macho na hii kitu ya uchifu. Uchifu kwa makabila mengi uliambatana na mamlaka juu ya ardhi na mara nyingi uliambatana na umwinyi.
Tuliondoa uchifu ili kuweze kuthibiti fulsa ziweze kupatikana kwa wote na kuimarisha demokrasia.
Uchifu pia uliambatana na baadhi ya mila mbaya za kunyanyasa wanawake na makundi fulani kwenye jamii. Utulivu ulikuepo kwa kua kila mtu alitii mamlaka ya chief japo hali ni kandamizi kwa baadhi ya mambo.
Kwa upande wa wasukuma hadi leo uchifu/ utemi unalinda imani za kishirikina na imani zinazokinzana na maendeleo. Waganga wa kienyeji usukumani ni utapeli mtupu.
Karibu uganga wote wa kienyeji ni chonganishishi. Ukiwapa fulsa waganga wa kienyeji kwa kisingizio cha uchifu watapata sapoti kisaikolojia.
Tutaona mauaji wa wazee mauaji ya albino na maovu tele yaliyopungua kwa kiasi kikubwa yakirejea.
Hii kitu ya uchifu tukae nayo mbali kabisa. Badala yake tufanye mambo ya kisayansi kuendeleza jamii. Utamaduni tuendelee kuulinda lakini sio kupitia machifu na watemi kama wale wa usukumani.
Wapinga maendeleo wapo kazini kupitia kila kona. Samia awe macho ili tusianzishe mambo ya kukwamisha maendeleo na umoja wa kitaifa ambao kwa sasa uko imara