Mambo makubwa ya Tupac Amaru Shakur enzi za uhai wake (1971-1996)

Mambo makubwa ya Tupac Amaru Shakur enzi za uhai wake (1971-1996)

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
MAMBO YA TUPAC AMARU SHAKUR (1971-1996)

Watu timamu wanaulizana...Ilikuwaje na ni kwa namna gani Tupac Amaru Shakur, kijana wa Marekani mwenye asili ya Kiafrika kufanya mengi na kupandikiza itikadi ama legacy kubwa mno pamoja na kuacha historia ndefu mno na alifariki akiwa na miaka 25 tuu😃 Alizaliwa 1971 na akauwawa 1996 kwa kupigwa risasi,huko Marekani!!

Mambo mengi hususani kwenye muziki wake aliyafanya kwa muda wa miaka 3-5 katika kipindi cha umaarufu wake ingawa muziki aliuanza akiwa shuleni akiwa na miaka 17+ alipojiunga na kikundi cha muziki kiitwacho Digital Underground mwaka 1989.

Aliishi katika kundi hilo hadi kutoa Albamu (Solo Album) yake ya kwanza ya 2Pacalypse mwaka 1991 ambayo ilitambulika na kusikilizwa kimataifa😃

Tupac ana albamu nne ambazo nyingine alizitoa wakati wa uhai wake na nyingine 7 zilitolewa baada ya kifo chake...

Enzi ya uhai wake alitoa albamu nne tuu ambazo ni 2Pacalypse Now (1991), Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z. (1993), Me Against the World (1995), All Eyez on Me (1996) na nyingine zipatazo 7 zilitolewa baada ya kifo chake!!.

Nyimbo zake nyingi alijikita katika kusawiri maudhui na maudhui yake yalikuwa na mchanganyiko wa maumivu ya kibinafsi, changamoto za kijamii, na harakati za kupigania haki, haswa haki za Wamarekani weusi (Negroes/Nigga) dhidi ya madhalimu ya Wazungu huko Amerika!!

Kiujumla ni kuwa, Kipindi alichoishi ni kifupi sana ukilinganisha na mambo mengi sana aliyofanya pamoja na itikadi pia na historia aliyoiacha!!

Huyu alikuwa ni Icon katika mziki wa Hip Hop ila hakuwahi shinda grammy sasa sijui ilikuwaje🙄

Tujaribu ku-share historia yake tuisome tuone ni mbinu gani alizitumia licha ya kuwa ana kipaji...Ila ni wangapi walikuwa na vipaji na wakaishi miaka zaidi ya 30 ila hawajaacha legacy kubwa kama yake🙄

Hebu tujaribu ku-share mawazo hapo kwenye comments...ALIFANYAJE KUFIKIA HATUA ALIYOFIKA!?
Ni mimi ndugu mwandishi Dogoli kinyamkela
1732375283182.jpg
✍🏾 😁​
 
Bila kusahau ndio msanii wa hiphop mwenye nyimbo nyingi akifuatiwa na Lil Wayne!
Kitambo kidogo niliwahi kusikiliza Album zake kuanzia asubuhi mpaka jioni!!

Alafu nyimbo zake nyingi ni anarap mwenyewe!
 
Huko kwa wenzetu toka zamani kijana wa miaka 25 ni kawaida kukuta ameshafanya mengi makubwa na kuacha legacy hata baada ya kufariki, ila huku kwetu kijana wa miaka 25 utakuta ni marioo na mlamba lips anayeishi kwa kulelewa na mishangazi, akijifariji kuwa bado ni mdogo hivyo akihitaji kuoa ndio ataanza kuwa serious na maisha
 
Huwa nashangaa kuona mashabiki wanamlilia msanii akiwa ana perform ila niseme tu ukwel ambao sijawahi mwambia mtu yoyote, kama ningefanikiwa kuona live show ya Huyu Mwamba, ningebubujikwa na Machozi kama Farmboy Luca wa Mama mzazi...
The Guy is a hiphop messiah na his songz are true definition of "ghetto gospel". He was brilliant and very charismatic, the realest nigga in the hiphop world.
And if Didy had anything to do with his demise, then lem get this straight, he deserves every "f..k u" that he is going through ryt now and so much more..
 
Back
Top Bottom