Mambo manne makuu ya kuyafahamu wakati wa kutafuta Scholarship

KingOligarchy

Senior Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
139
Reaction score
375
Udhamini (scholarships) ni zawadi hivyo mtu akipata hana jukumu la kuilipa , Duniani kuna aina mbalimbali za udhamini zaidi ya maelfu kwa maelfu , zikitolewa kwa vigezo mbalimbali kama vile Watu binafsi , Mashule , Dini , Mashirika ya kijamii , Makampuni n.k
Kabla ya kutafuta udhamini wowote kuna maswali makuu matano ambayo unapaswa kuyatatua majibu yake , Maswali yenyewe na majibu yake ni kama ifuatavyo:

Ø KUNA AINA NGAPI ZA UDHAMINI ZINAPATIKANA
Kunaudhamini wa vyuo vikuu unaotolewa kulingana na SIFA (Merit based), Mtu anaweza kudhaminiwa endapo pale atafikia au kuvuka sifa zinazotakiwa ili kupokea udhamini huo kutoka kwa Mdhamini. Udhamini huo unaweza kutumia vigezo vya ufaulu wa elimu au pia kutumia ufaulu a elimu na kipaji cha muombaji (Mfano. mcheza mpira), jinsia n.k na aina nyingine ni ule unaoangalia vigezo wa uhitaji wa kifedha (Financial Need)

Aina nyingi za udhamini hulenga makundi mbalimbali katika jamii kama vile udhamini wa wanawake au udhamini wa wanafunzi waliomaliza sekondari (High School Seniors) na nyinginezo zikiangalia eneo na aina ya kazi ya wazazi wanapofanya kazi mfano ; Wanajeshi

Udhamini unaweza kuwa wa aina mbalimbali , unaweza ukadhaminiwa kulipiwa kila kitu kitachohusisha elimu kama vile malazi , Ada , chakula , insurance na pia usafiri wa ndege wa kwenda na kurudi na kilinda mfuko au unaweza ukapewa udhamini wa pesa kidogo ili kupunguza ukali wa maisha , Lakini kwa kuangalia njia zote ni bora kuomba udhamini sababu itapunguza gharama ya masomo yako.

Ø NI LINI MUDA MUAFAKA WA KUOMBA UDHAMINI?
Jambo hili mara nyingi hutegemea na siku ya kuomba udhamini , Ni vizuri kuanza kutafuta udhamini mwaka mmoja kabla ya chuo kuanza , kwahiyo kama upo chuo ni muda mzuri wa kuanza kujiandaa , kuchagua na kuomba udhamini .

Ø JINSI GANI YA KUOMBA UDHAMINI?
Kila udhamini una matakwa yake , Hivyo basi kupitia tovuti yenye udhamin husika maelezo yote yatapatikana namna na jinsi ya kuomba udhmini husika . Unatakiwa kusoma na kuyajaza maombi yako vizuri , na kasha kuyatuma kabla ya siku ya mwisho



Ø JINSI YA KUPATA PESA ZILIZOTOLEWA NA MDHAMINI
Inategemea na udhamini. Pesa inaweza ikatumwa kwenda chuo ambacho ulichoombea inaweza ikawa ada ,ama deni ambalo hujamaliza kulilipa na hela zilizobakia kukabidhiwa kwako na chuo au unaweza ukatumiwa hela kwa mumo wa cheki. Mdhamini anatakiwa kutoa taarifa ya nini utegemee baada yaw ewe kuchaguliwa kufaidika na udhamini, endapo hujapata taarifa hizi hakikisha unaulizia mapema


JE UNA GPA NZURI (3.8/5) UNATAKA KUPATA SCHOLARSHIP?? WASILIANA NA MIMI KUPITIA brightonross@live.com NIKUSAIDIE BUREEEEEEEE *NO STRINGS ATTACHED
 

Attachments

Gpa ya 3.0 vipi naweza nikapata
 
unawasaidia scholarship wanaoenda kusoma PHD au MA? na vip kwa wenye lower second huwez kuwasaidia maana for international recognized gpa ni 2.7 wanaweza soma MA?
 
kwa nini uombe kwa mwaka unafuata maana huwa naona katika vyuo vyote dunia kuna intake mbili (march na september intake)tu kwa mwaka uliombea na si kwa mwaka unaokuja kama ulivyoandika
 
Mkuu kwa scholarship zinazoangalia kiwango cha ufaulu Hapana , Labda aina nyingine za scholarships ambazo ni chache na zina competition kubwa mfano. scholarship zinazotolewa kwa kuangalia talents etc
 
Kupata scholarship sio lazima , ni competition so huwez kujua ni zipi ambazo utapata lakini ukianza kujiandaa mda mrefu unapata chance kubwa ya kuchaguliwa na kupewa udhamini sehemu mbalimbali , unaweza ukaomba scholarship hata ya intake ya the same year nakubaliana na wewe ila ukitaka kuwa na uhakika zaidi ni vizuri kuanza kujiandaa mapema
 
Nasaidia kwa wote wanataka udhamini kuanzia degree , Ma na PHD. mwenye Gpa ya 2.7 anaweza soma M.a ila ni vigumu kupata ufadhili/ scholarship , kitu ambacho anachoweza kujaribu ni kujilipia chuo halafu akiwa bado yuko chuoni akatafuta kazi na kujilipia lakini bado ugumu upo mkubwa (work-study jobs) ,
 
Yaan bro umenigusa penyew nilikuwa natafuta sana kwenda kusoma nje sema pa kuanzia ilikuwa ni shida.tuwasiliane basi mkuu
 

Yaani umenigusa penywe bro waweza ni pm namba ako ili tuwasiliane
 
nina GPA ya 3.0 Bsc-ed!naweza pata udhanimi?nataka ningepata mambo yagesigesi!!!!
 
Mi nina gpa ya 3.6 kwenye Bed (arts), je nitaweza kupata scholarship nisome masters ya english?
 
ZINGATIA MAMBO YAFUATAYO, (Muendelezo....)


ü Vyeti vya Lugha (Certificate of Language Proficiency)
Baadhi ya udhamini huwa wanataka muombaji kufika steji flani katika lugha ngeni (foreign language), kwa watanzania lugha ya Kiingereza inakuwa ni lugha ngeni sababu kiswahili ndio lugha mama hivyo basi inatakiwa kufanya mitihani mbalimbali ya lugha Mfano. TOEFL ( Test of English as a Foreign Language) , IELTS (International English Language Testing System), ESL (English as a second Language).
ü CV (curriculum Vitae)
Muombaji pia anatakiwa kutuma cv inayoonyesha elimu aliyopata na uzoefu wa kazi(kama upo) , cv yako inapaswa kuonyesha harakati za elimu pamoja na maisha binafsi kama vile fani, michezo , lugha , Uwezo wa computer n.k
ü Uthibitisho wa Uraia ( Proof of citizenship)
Muombaji wa udhamini anapaswa pia kutoa uthibitisho wa uraia wake pale anapoomba udhamini kwa kuonyesha nyaraka zifuatazo
· Paspoti ya kusafiria (Travelling Passport)
· Cheti cha kuzaliwa (Birth Certificate)

ü Vyeti halisi vya Elimu (Academic Transcript)
Muombaji wa udhamini anapaswa kuhakikisha anatoa vyeti vilivyokuwa vimekuwa vimehakikiwa na mwanasheria (Certified) kwa masomo yote aliyosoma,Vyeti hivyo vinatakiwa vionyeshe Alama za ufaulu mfano. 90% au Grade A, Vyeti vinavyotumia alama za ufulu kama 86% na GPA 3.8/5 au GPA 3.5/4 ndizo ambazo hupendelewa kutumika kwenye kuomba udhamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…