Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kama wanadanamu hatuwezi kuishi kila siku kwa namna moja au kuwa na furaha muda wote au kuwa na mambo mazuri siku zote, bali kuna nyakati ambazo tunakutana na mambo ambayo hatuyatarajii kabisa
Sasa haya mambo ambayo hatuyatarajii ingawa tunajua yanaweza kutokea muda wowote ule basi nakuletea mambo manne ambayo ukikutana na hali hiyo basi uweze kudili nayo
Mosi,kukiri kwanza jambo fulani lisilo kupendeza limetokea, inaweza kuwa ajali, maradhi, kufukuzwa kazi, kuachwa nakadhalika, kukiri kwamba umetokewa na jambo hilo ni njia ya kukupa utulivu
Mbili,kukubali hali hiyo kwamba imetokea au imekutokea,kitendo hiki ni njia ya kiroho ambayo itakusaidia kutoka kwenye machungu na maumivu na kukupeleka kwenye utulivu wa nafsi, kubali kwamba wewe ni HIV positive kwa maana ishatokea tayar huwezi kubadili hali hiyo cha kufanya ni kuikubali hali hiyo
Kubali kwamba mahusiano yamefika mwisho umeachwa kwahiyo ipokee hiyo hali kama ilivyo, kubali kazi umeachishwa ndo ishatokea sasa huwezi kurudisha siku nyuma, kwa kukubali hali hiyo hapo utapata utulivu na amani, usitafute mchawi we kubali tu kwamba ishatokea
Tatu, kubali kuingia katika mazingira mapya ili uondokane na hali iliyo kutokea au unafuu upatikane, hapa weka igo yako pembeni, ulikuwa na kazi nzuri sana sasa imeisha, acha kuishi kama mambo safi hapa ishi kutokana na mazingira ulinayo sasa, paki ndinga pembeni usiingie kwe mikopo ili uendeshe gari ambalo sasa huwezi kulihudumia, nenda kituo chukua dala dala fresh tu
Nne,hatua hii ndio nyepesi hasa baada ya kuzikubali hatua hizo tatu zilizo pita, nayo ni kufanya kwa vitendo sasa,ni wakati wa kukung'uka suruali au sketi na kusimama na kusonga mbele kwa vitendo, hapa sahau huzuni zote,ondoa maumivu yote na songa mbele, wanasema majaliwa yakifunga mlango wa mafanikio basi matumaini hufungua milango mipya ya mafanikio.
Ni hayo tu!