RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Kama bado unajitafuta kimaisha, hakikisha unaishi kwenye haya mambo matano (5);- SHAUKU, UDADISI, UKALI, KUBADILIKA, & USIRI.
1. SHAUKU
Kama unajitafuta ni vyema kuwa na shauku kubwa ya kufika mahali unapopataka. Usibaki kuwa na ndoto pekee ya mdomoni, akilini au kwenye makaratasi - bali anza mikakati ya kutimiza ndoto hiyo. Kama unataka kufika sehemu unayotaka kwenda, amka hapo ulipoketi kisha anza safari, na ukianguka amka tena. Usihofu udhaifu wako kwani kumbuka; "hata kwa mbawa zilizovunjika wakati mwingine unapata njia yako ya kuruka".
2. UDADISI
Binaadam ni vizuri uwe mdadisi kabla ya kuanza kufanya jambo lako. Kwa mfano; kama unataka kuanza biashara pesa pekee sio mtaji bali pia udadisi ni mtaji. Ni vizuri kujua ni biashara gani ufanye, eneo gani, wakati gani, na kwa ubora upi. Huo ni mfano mmoja tu, lakini yapo mambo mengi yanahitaji udadisi wako.
3. UKALI
Kuwa mkali kwenye mambo yako. Weka mipaka ya mazoea katika mambo yako, kama vile; mipaka ya urafiki dhidi ya pesa zako au mipango yako, mipaka ya kazi na mizaha. Jitahidi uwe mkali kwenye mambo ambayo hayako sawa hata kidogo. Kwa mfano kama kijakazi wako wa dukani/saluni/ mgahawani, n.k, ni mtu anayesababisha hasara kila siku kwenye biashara yako, hebu kuwa mkali, ikiwezekana mbadilishe haraka.
4. UWEZO WA KUBADILIKA
Uwe mtu mwenye utayari wa kupokea mapokeo mazuri wakati wowote. Usikaririwe kuwa wewe ni mtu ambaye huna kazi nyingine unayoiweza zaidi ya kazi fulani tu. Unapaswa kuwa mtu wa kubadilika na kujifunza haraka sana kwa manufaa mazuri.
5. USIRI
Siri ni jambo muhimu sana kwenye maisha yako. Kama pombe zinakufanya unatoa siri za mipango yako ya maisha, acha kunywa pombe haraka sana. Usiri na ukimya umezungumziwa pia kwenye kitabu cha (The 48 Laws of Power (Robert Greene) - Law No.4). Kuna njia mbili za kutunza siri zako.
Njia ya kwanza ni kuwa mkimya katika mambo yako. Njia ya pili ni kuongea ukweli usiolenga ukweli halisi wa mambo yako. Kwa mfano upo kwenye pikipiki unaelekea site kutazama ujenzi wa nyumba yako ghafla anakupigia simu mtu ambaye hutaki ajue kuwa unajenga, ukimwambia upo chumbani umelala ilhali anasikia sauti na upepo wa pikipiki utamfanya akuone muongo na ataanza kukupeleleza ni jambo gani unamficha, lakini ukimdhihirishia kuwa upo kwenye pikipiki na unakwenda ufukweni (beach) kupunga upepo atakubaliana na wewe. Kama ni mtu ambaye hapendi kuona unafanikiwa ataridhika na kufurahi pindi anaposikia kuwa mizunguko yako ni ya kupoteza muda (Ukweli usiolenga ukweli halisi).
Asante.
RIGHT MARKER - TZ