RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
💼 MHADHARA Na.5
Karibu kwenye Mhadhara wa tano. Leo nakuletea mambo makuu matano (5) ambayo yatamchepusha mkeo.
1. UGOMVI USIOKWISHA KWENYE NDOA.
Kutofautiana kwenye ndoa ni jambo la kawaida, lakini kuufanya ugomvi uwe chakula chenu cha kila siku ni fursa kwa vijana wanaomtamani mkeo. Kadiri unavyozidi kumsusa mkeo na kumuweka mbali kwasababu ya maugomvi ya kila siku, ndivyo unazidi kumsogeza mkeo karibu na wanaume wanaomtaka.
2. UCHEPUKAJI WA WAZI/MAKUSUDI.
Kama una tabia ya kuchepuka jifunze kuwa msiri. Kadiri mkeo anavyokufumania na wanawake wengine, au kila siku anasikia tabia zako mbaya za kuchepuka na wanawake tofauti - amini nakwambia vidume wenzako watamnyakua mkeo chapu kwa haraka, na hutosikia wala kumuhisi atakayekuibia mke kwasababu mkeo atajifunza kuficha siri kupitia udhaifu wako wa kutoficha siri.
3. POMBE/ULEVI.
Hapa naomba unielewe vizuri. Pombe kama pombe haziwezi kumfanya mkeo achepuke. Mkeo hawezi kuchepuka eti kwasababu unakunywa pombe. Lakini kama pombe zitakufanya uwe na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani kwako usiku, au kufanya fujo ndani kwako, au kutoacha hela ya matumizi, au kero yoyote- Amini nakueleza hizo tabia zitakazoibuliwa na pombe/ulevi wako zinaweza kumpeleka mkeo kwa mwanaume mwingine.
4. UBINAFSI/UCHOYO.
Mwanaume usiwe mbinafsi kwenye familia yako. Kama huna onyesha kweli huna. Ubinafsi ninaouelezea hapa ni kama vile; kujipendelea kujinunulia vitu vizuri mfano nguo nzuri, viatu vizuri, simu za gharama, au unampiga marufuku mkeo kupanda gari lako. Au unarudi nyumbani kwako unacheuwa kuku wa hotelini, hutaki kula dagaa uliowaacha ndani kwako na mkeo anagundua huko ulikotoka umekula kuku. (Bila kujali kipato chako ni kikubwa au kidogo acha ubinafsi, kama hulka yako ni kuvaa vizuri hakikisha mkeo pia anavaa vizuri. Ni bora ijulikane pesa unafanyia mambo ya msingi kuliko kila siku unabadilisha simu za gharama halafu mkeo huu ni mwaka wa tano anamiliki Kitochi cha elfu 18 kimefungwa mpira - Amini nakwambia atapelekewa moto nje na huko nje hapewi chochote.
5. KUMNYIMA HAKI YAKE YA NDOA KWA MAKUSUDI.
Mkeo anaweza kuvumilia kama anakosa haki yake ya ndoa kwasababu umgonjwa. Lakini kama unamnyima mkeo haki yake ya ndoa (kwa makusudi) kwasababu ya ugomvi usiokwisha, au kumchoka, au unachoshwa na penzi la michepuko, au unamwona mkeo ni kama dada yako - Amini nakwambia mwezi ujao hautokwisha utaibiwa.
BY: RIGHT MARKER-TZ
Mhadhara wa 5.
Sept 18, 2024.