Uchaguzi 2020 Mambo matatu aliyozungumza Profesa Kitila Mkumbo leo Makurumla

Uchaguzi 2020 Mambo matatu aliyozungumza Profesa Kitila Mkumbo leo Makurumla

Joined
Oct 7, 2015
Posts
86
Reaction score
108
Mgombea ubunge wa jimbo la ubungo kupitia Chama Cha mapinduzi Profesa Kitila Mkumbo amezungumzia Mambo matano muhimu atakayoanza kuyashughulikia punde tu akiapishwa kuwa mbunge.

Profesa Kitila Mkumbo amesema
"Nina usongo na kuwa mbunge. Nikiapishwa tu naanza kupambana na kero za wana Ubungo haraka iwezekanavyo"

1. Nitaanza na barabara za mitaani. Rais ameshaahidi kutujengea na kazi yangu itakuwa kufuatilia

2. Tutashughulika na mafuriko ya Mto China. Tutajenga kingo imara za mto China na wananchi wataepuka kero za mafuriko ya mara kwa mara

3. Kuboresha Kituo cha Afya cha Makurumla,Kituo hiko kitafanya kazi kwa muda wa saa 24.
Utaratibu wa kuzuia maiti hospitalini kwa sababu ya kudaiwa utakomeshwa. Rais Magufuli ameshatoa uamuzi. Msingi wa kwanza wa CCM ni utu. Hili halitaendelea
IMG_20201023_172523_393.jpg
IMG_20201023_153700_974.jpg
 
Usaliti mbaya sana Jamani.

Na dhambi ya usaliti ni Mbaya sana jamni
 
Huyu jamaa chenga sana. Huyu alikua anaongea vitu vya maana sahivi sijui anaongeaga nini
 
Siasa za bongo bana,miaka nenda rudi bado wanazungumzia maji etc
2025 tena wakirudi Wanasiasa watarudi na mwimbo wenye biti hili hili

Ova
 
Huyu jamaa chenga sana. Huyu alikua anaongea vitu vya maana sahivi sijui anaongeaga nini
Tatizo lenu 'Wapuuzi' wachache huwa mnapenda Kuyasikia yale mnayoyataka nyie 'Wapinzani' ila yakiwa ni ya 'CCM' msiyoipenda mnachukia sana.
 
Tatizo lenu 'Wapuuzi' wachache huwa mnapenda Kuyasikia yale mnayoyataka nyie 'Wapinzani' ila yakiwa ni ya 'CCM' msiyoipenda mnachukia sana.
Huo upinzani unanipa wewe. Serikali yoyote inayojali watu wake haiwezi kununua ndege 'keshi' halafu maji inasubiri udhamini wa 'mabeberu' . Fikiri kuhusu hili jiulize wewe na Mimi nani 'mpuuzi' .
 
Huyu jamaa chenga sana. Huyu alikua anaongea vitu vya maana sahivi sijui anaongeaga nini
Inawezekana toka mwanzo alikuwa haongei vitu vya maana,pengine wewe ulikuwa unaona anaongea vitu vya maana kwa sababu ni vitu ambavyo ulikuwa unapenda kuvisikia wakati huo na kutokana na upande aliyokuwepo wakati huo.
 
Inawezekana ukawa sahihi. Lakini mafuriko dar hayatokea mwaka/msimu huu tu. Ni kila mara inyeshapo mvua. Lakini serkari haijatafuta suluisho la kudumu. Angalau sasa wangekua wanaahidi kujenga kingo zilizovunjwa na mvua. Lakini ndio kwanza wanaahidi kujenga(kumbuka Ni ahadi hii).
 
Huo upinzani unanipa wewe. Serikali yoyote inayojali watu wake haiwezi kununua ndege 'keshi' halafu maji inasubiri udhamini wa 'mabeberu' . Fikiri kuhusu hili jiulize wewe na Mimi nani 'mpuuzi' .
Kwa hiki ulichoendelea 'Kukiandika' hapa nikikuita 'Mpuuzi' bado tu nitakuwa nakosea au ninakukosea? Imarisha Kwanza 'IQ' yako ujadiliane nami.
 
Back
Top Bottom