BIG Africa
Member
- Oct 15, 2022
- 85
- 118
Habari wadau wa JF.Kwanza kabisa mimi sikuwepo wakati vita ya Kagera(1978-1979).Nilikuwa bado sijazaliwa.Lakini kupitia kutazama mikanda ya ya video ya Vita ya Kagera iliyopo YouTube na kwenye CD kuna mambo mawili nimejifunza katika vita hiyo.Mambo gani hayo?.JAMBO LA KWANZA nchi yetu ya Tanzania ilikuwa bado ina uchumi mbovu sana.Ukitaka kubaini dhana ya kiuchumi kwa wakati huo tazama magari ya kivita,silaha,maisha ya kiujumla kwa wananchi wa Tanzania,hata mavazi ya askari(kombati) utagundua vitu hivi vyote vilikuwa ni duni.Hali hii ilitokana na hali halisi ya kwamba mwaka 1978 wakati vita ya Kagera inaanza Tanzania ndio ilikuwa ina miaka 16 tu tangu ipate uhuru.Kwa hiyo kiuchumi ilikuwa inajitafuta.Ukitazama vizuri video za vita ya Kagera kuna askari mmoja huwa anaonekana anatoa mafunzo ya kijeshi kwa mgambo/raia akiwa amevaa raba aina ya "Converse".Inachekesha.JAMBO LA PILI nililojifunza miaka hiyo Watanzania walikuwa ni "wazalendo" sijawahi kuona katika kizazi chetu hiki.Kiufupi hali ilikuwa ni tofauti.