Mambo mengi ya Serikali yetu yanafeli kwasababu ya wanaoyaendesha ni wasomi

Mambo mengi ya Serikali yetu yanafeli kwasababu ya wanaoyaendesha ni wasomi

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
748
Reaction score
367
Ukifuatilia wenye mafanikio makubwa Sana hapa nchini ni watu wa kawaida Sana kielimu.

Hii unamaanisha kwamba tangu siku walipogundua kwamba hawana elimu kubwa waliamua kujisemea moyoni kwana natakiwa kua na vitu vikuu vitatu:

UWAJIBIKAJI
UAMINIFU
NIDHAMU YA FEDHA

Haya ndio Mambo tunayo wazidi wasomi. Ukitaka kuamini fanya utafiti wa aina ya maisha anayoishi msomi mwenye hela na asie msomi mwenye hela utajua ninacho maanisha na Kama hutaelewa comment hapo chini ili niendelee kukushibisha kwenye comment.

Naitwa
Matendo Andrew mgeni
Rais wa wana darasa la saba Tanzania.
 
Halihitaji Phd kugundua hilo, matajiri wengi shule hawana.. serikalini nahisi ni mfumo tuu uliwekwa ila mwisho wa siku kila kitu kina sehemu yake
 
Hesabu ni msingi wa kila kitu. Mahali. Takwimu zinasaidia kugundua idadi ya waliopata madhara au maradhi na serikali inaweza kuweka pesa kufanya tafiti na kuona nini kifanyike.

Takwimu zinapopikwa ni mwanzo wa msingi mbovu na usitegemee nyumba kusimama.
 
Mpaka siku tutakapogundua lengo hasa la elimu hii ya mzungu ni nini tutaendelea kuhangaika tu yaani....

Kama mafanikio unayoongelea ni utajiri ni ukweli wa jumla kuwa karibu duniani kote matajiri wakubwa siyo wasomi (wabobevu).

Unafikiri ni kwa nini?

Na kule ilikotoka elimu hii watu wala hawahangaishwi na hili ndiyo maana hata profesa hawamtegemei awe tajiri. Pengine ndiyo maana akina Albert Einstein walikufa masikini tu...japo walifanikiwa sana kwa walilotakiwa kufanya. Huku Afrika naona wangechekwa sana kwa kufa bila "kufanikiwa"

➡️➡️➡️ Lengo la hii elimu ya mzungu siyo kuwatajirisha waipatayo. Na kama unataka mtoto wako awe tajiri elimu ya fomu foo (au siksi) inamtosha. Baada ya hapo mpe mtaji aingie mtaani akapambane!

...ila tunahitaji walimu. Tunahitaji madaktari. Tunahitaji wanasheria. Tunahitaji walinzi. Tunahitaji mapolisi na wanajeshi. Tunahitaji wasomi...hata kama hawatafanikiwa (hawatatajirika)

Pengine dhana yetu ya mafanikio ina matatizo. Pengine lengo la hii elimu yetu hatulijui...

Kuna tatizo mahali!
 
Ukifuatilia wenye mafanikio makubwa Sana hapa nchini ni watu wa kawaida Sana kielimu.

Hii unamaanisha kwamba tangu siku walipogundua kwamba hawana elimu kubwa waliamua kujisemea moyoni kwana natakiwa kua na vitu vikuu vitatu:

UWAJIBIKAJI
UAMINIFU
NIDHAMU YA FEDHA

Haya ndio Mambo tunayo wazidi wasomi. Ukitaka kuamini fanya utafiti wa aina ya maisha anayoishi msomi mwenye hela na asie msomi mwenye hela utajua ninacho maanisha na Kama hutaelewa comment hapo chini ili niendelee kukushibisha kwenye comment.

Naitwa
Matendo Andrew mgeni
Rais wa wana darasa la saba Tanzania.
Nafikiri ni kinyume chake, wajinga ndio wanaongoza nchi hii na ndio maana mambo yapo hovyo.
 
Back
Top Bottom