Mambo muhimu ili ufanikiwe katika maisha

Mambo muhimu ili ufanikiwe katika maisha

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
Good Luck
Hawa ndio wale watu ambao hushinda Biko, Jackpot, kubahatika kupata scholarship na vile vitu ambavyo kwa nguvu ya kawaida ni ngumu kuamini kuwa mtu angefanikiwa kupata hicho kitu.

Kuwa na kipaji pia inaambatana na kuwa na bahati njema maana si kila mtu amebahatika kuwa na kipaji.

Pia hata kuzaliwa kwenye familia iliyobarikiwa kifedha, status nzuri ya maisha nayo ni bahati.

Beauty
Hapa ni uzuri wa aina zote, uzuri wa sura, uzuri wa maumbile, uzuri wa tabia, uzuri atika jambo fulani utakusaidia wewe kufungua milango ambayo wengine watashindwa ifikia.

Mfano, uzuri wa sura husaidia mtu kupata kazi kama za kuwa mtangazaji katika television, uzuri wa sauti humsaidia mtu kupata kazi katika utangazaji wa radio ama kuwa customer care, uzuri wa tabia humsaidia mtu kupata kazi kama mwalimu, nk

Intelligece
Hapa nazungumzia akili za darasani, maisha, ufundi, utundu wa kimaendeleo.

Ukiwa na akili za darasani ni rahisi kuanza kupata kazi kama mwalimu wa tuition hata kabla hujamaliza shule, ni rahisi kuwa mwandishi wa vitabu.

Ukiwa na akili za maisha hii itakusaidia sana kuweza kuwa mfanya biashara bora bila hata kutumia elimu ya darasani.

Ukiwa na akili za ufundi (kutumia viungo vyako) hii itakusaidia kuwa fundi bora na kuweza kuishi vizuri na kujipatia kipato.

Ukiwa mtundu, hii itakusaidia pia kufika mbali, mfano kuna watu wamebarikiwa na utudu wa kuweza kutengeneza vifaa vya umeme. Kwaio mtu kama huyu akibahatika akapata elimu zaidi na akapata sehemu ambayo itamuendeleza vizuri basi anaweza akafanya mambo makubwa sana.

Hivyo basi, kama Mungu amekujalia kuwa na hivi vitu vyote wewe ni mwenye bahati kubwa sana, kama Mungu amekujalia kimoja wapo pia wewe ni mwenye bahati, na kama unahisi hauna hata kimoja basi tengeneza uzuri wa tabia.

Mwisho kabisa, juhudi ni muhimu sana, unaweza kuwa na bahati, mzuri na unaakili lakin uvivu wako utamfanya kila mtu akuone hufai. Tuombe Mungu atujalie tuwe na vizazi vyenye bahati njema, uzuri na akili. Ameen

Wanasema kwenye maisha ukifika umri wa miaka 20 unatakiwa uanze kujipima.

Je, vitu vyako huwa vinakuja kwa namna gani?

Vinatokea tu kwa kutumia nguvu sana au vinakuja wakati ambapo hutarajii?

Basi ukishapata jibu litakusaidia kutokuwa na stress na anxiety. #beauty #intelligence #lucky #success
 
Sawa, ila kiuhalisia sivyo! Aliyekuwa wa mwisho darasani leo hii ni tajiri! Professor anamuomba beer! Imekaaje?? Huenda kufanikiwa ni "maujanja"

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo nadhani kaiweka kwenye kundi la bahati pia ameiweka kwenye kundi la uzuri. Naweza nisiwe mzuri darasani nikawa mzuri katika mchezo wa mguu
 
All in all, connection, katika dunia ya sasa hicho ndo kitu muhimu....mjini ukikosa connection utasumbuka Hadi maiti yako kutolewa mortuary, na eneo la kuzikiwa pia utapata kwenye maporomoko mvua ikinyesha kaburi lako linasombwa... CONNECTION!
 
Hata mchezo wa mpira kuna maujanja, ni kwa vile tu hujui. Wewe amini maisha ni "mchezo" na mafanikio ni Siri ya mtu. Kuna mtu kalima eka Moja ya mahindi na nwenzake jirani kalima eka Moja.

Kila mtu alitumia utaalamu wa kutosha na udongo ni uleule. Mmoja akavuna gunia 10 mwingine gunia 1. Kumbuka hakuna aliyefanya uzembe.

Hapo Kuna nini? Unaweza ukawa mchezaji mzuri ila kila ukicheza unaona mipira miwili na unapiga ule mpira fake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubarikiwe mkuu.. nilishawahi kufika office flani na mimi sikuwa mkusudiwa nilimsindikiza jamaa yangu mmoja kukamilisha/kuhangaikia mambo yake ya vyeti vya form six banah tulikuta maoficer wengi tofauti tofauti .

Cha ajabu walianza kunifurahia na kuniimbia na kunipisha kwenye kitu cha mkuu wao hapo officen nikae mimi na kunichangia pesa kadhaa na tuliangaikiwa shida yetu haraka sana .. niliona kama walikuwa wakinitania ila walisema wamefurahi kuniona sana wakati hata siwafahamu.. maisha banah daah
 
All in all, connection, katika dunia ya sasa hicho ndo kitu muhimu....mjini ukikosa connection utasumbuka Hadi maiti yako kutolewa mortuary, na eneo la kuzikiwa pia utapata kwenye maporomoko mvua ikinyesha kaburi lako linasombwa... CONNECTION!
...ni kweli 'Connection' ni muhimu kiasi hicho? Au ni sisi wenyewe tumeipa huo umuhimu (tumeikuza mno)?
 
Ubarikiwe mkuu.. nilishawahi kufika office flani na mimi sikuwa mkusudiwa nilimsindikiza jamaa yangu mmoja kukamilisha/kuhangaikia mambo yake ya vyeti vya form six banah tulikuta maoficer wengi tofauti tofauti cha ajabu walianza kunifurahia na kuniimbia na kunipisha kwenye kitu cha mkuu wao hapo officen nikae mimi na kunichangia pesa kadhaa na tuliangaikiwa shida yetu haraka sana .. niliona kama walikuwa wakinitania ila walisema wamefurahi kuniona sana wakati hata siwafahamu.. maisha banah daah
Bahati hizo mkuu,una nyota ya kupendwa sana mzee 😅
 
Kwenye mafanikio kuna mambo mawili “JUHUDI” na “BAHATI” hivyo viwili lazma viende sambamba ndipo utafanikiwa. Juhudi ndio huzalisha “CONNECTIONS” ila pia hazitakusaidia kama huna bahati!

Ukiwa mtu wa juhudi sana ila huna bahati mwishowe utaanza kumtafuta mchawi nani!Mtu Connection anapata ila mikingamo inatokea unakuta mtu hafanikiwi zinaanza tu blah blah za hapa na pale CV inazungushwa mara vitu havieleweki yani acheni tu.

Mtu kasoma ana GPA za 4.5 na ni kipanga kweli miaka yote ila anaishia kukata kata matunda barabarani😎 wakati kimsingi mnaomfahamu mnaona alistahili kuwa TPDF kabisa au NSSF katika nafasi za juu. Maisha ni fumbo kuu

Sikatai yapo mazingira ambayo mtu anaweza kuwa amefitiniwa na nguvu flani hasi toka kwa watu wenye husda. Unakuwa umefungwa kimazingira yani mafanikio yako yatakuja kwa ugumu sana. Au usifanikiwe kabisa ukawa unaishi kawaida tu kula kulala maendeleo 0!

Pamoja na yote bahati tu ukiwa nayo unanyoosha maisha vizuri mno. Kuna watu wamekuwa average toka shule mpaka chuo ila wakatoka uraiani wakapokelewa vyema na kitaa na wakatoboa fasta mno!
 
Bahati hizo mkuu,una nyota ya kupendwa sana mzee [emoji28]

Aaa mkuu.. yaani pengine kuna sehemu unapata tabu na shida nyingi ila kuna sehemu unatafutwa ukawe MFALME.. daah maisha haya wewe acha tu [emoji23]
 
Kwenye mafanikio kuna mambo mawili “JUHUDI” na “BAHATI” hivyo viwili lazma viende sambamba ndipo utafanikiwa. Juhudi ndio huzalisha “CONNECTIONS” ila pia hazitakusaidia kama huna bahati!

Ukiwa mtu wa juhudi sana ila huna bahati mwishowe utaanza kumtafuta mchawi nani!Mtu Connection anapata ila mikingamo inatokea unakuta mtu hafanikiwi zinaanza tu blah blah za hapa na pale CV inazungushwa mara vitu havieleweki yani acheni tu.

Mtu kasoma ana GPA za 4.5 na ni kipanga kweli miaka yote ila anaishia kukata kata matunda barabarani[emoji41] wakati kimsingi mnaomfahamu mnaona alistahili kuwa TPDF kabisa au NSSF katika nafasi za juu. Maisha ni fumbo kuu

Sikatai yapo mazingira ambayo mtu anaweza kuwa amefitiniwa na nguvu flani hasi toka kwa watu wenye husda. Unakuwa umefungwa kimazingira yani mafanikio yako yatakuja kwa ugumu sana. Au usifanikiwe kabisa ukawa unaishi kawaida tu kula kulala maendeleo 0!

Pamoja na yote bahati tu ukiwa nayo unanyoosha maisha vizuri mno. Kuna watu wamekuwa average toka shule mpaka chuo ila wakatoka uraiani wakapokelewa vyema na kitaa na wakatoboa fasta mno!

Naam MKUU.. ni sahihi
 
Back
Top Bottom