Kuna watu humu walikuwa hawajui kuwa mahusiano ya kimapenzi ni hiari.
Mwaka jana niliandika mada humu kuhusu kuhisi demu wangu kumegwa alipoenda kumpeleka mwanae nchi nyingine kwenda kumuona baba yake. Watu walinistaajabisha sana! Eti wakawa wanahoji kwa nini nilimuachia aende?
Alaa! Zaidi ya mimi kupinga yeye kwenda ningemzuiaje sasa kama alikuwa kanuia kufanya hivyo kwa gharama yoyote ile? Ningemfunga kamba asiweze kutembea? Kifikra watu tumetofautiana sana. Sasa kumbe hata sheria yetu ya ndoa inalitambua hilo la hiari!
Kwenye mahusiano ya kimapenzi huwezi ukamzuia mwenza wako kufanya kitu ambacho anataka zaidi ya kupinga kwa maneno. Huwezi ukamchapa viboko au ukamdunda mangumi (ingawa wapo wafanyao hivyo lakini hayo yote hayasaidii chochote kama mtu kanuia kufanya kitu) na kudhani eti indo umefanikiwa kumkataza. Akiamua kufanya kitu atafanya tu.
Sasa cha msingi ni wewe utachukua hatua gani baada ya yeye kukiuka matakwa yako. Nilikuwa sahihi mwaka jana nab ado niko sahihi leo hii na nitaendelea kuwa sahihi kuwa mapenzi si utumwa na utwana. Mapenzi ni hiari!
Mahusiano yoyote yale na hasa ndoa ni hiari. Hupaswi kumlazimisha mtu. Ndo maana sheria yetu ilipoona ukorofi wa wanaume wakiafrika na ubabe
wetu ikaweka wazi kuwa ndoa ni hiari. Kutokana na tabia iliyokuwepo miaka ile sheria ikatamka wazi kuwa ni kosa kumchapa mwenza wako viboko.
S. 66. For the avoidance of doubt, it is hereby declared that, notwithstanding any custom to the contrary, no person has any right to inflict corporal
punishment on his or her spouse.
Kuna watu humu walikuwa hawajui kuwa mahusiano ya kimapenzi ni hiari.
Mwaka jana niliandika mada humu kuhusu kuhisi demu wangu kumegwa alipoenda kumpeleka mwanae nchi nyingine kwenda kumuona baba yake. Watu walinistaajabisha sana! Eti wakawa wanahoji kwa nini nilimuachia aende?
Alaa! Zaidi ya mimi kupinga yeye kwenda ningemzuiaje sasa kama alikuwa kanuia kufanya hivyo kwa gharama yoyote ile? Ningemfunga kamba asiweze kutembea? Kifikra watu tumetofautiana sana. Sasa kumbe hata sheria yetu ya ndoa inalitambua hilo la hiari!
Kwenye mahusiano ya kimapenzi huwezi ukamzuia mwenza wako kufanya kitu ambacho anataka zaidi ya kupinga kwa maneno. Huwezi ukamchapa viboko au ukamdunda mangumi (ingawa wapo wafanyao hivyo lakini hayo yote hayasaidii chochote kama mtu kanuia kufanya kitu) na kudhani eti indo umefanikiwa kumkataza. Akiamua kufanya kitu atafanya tu.
Sasa cha msingi ni wewe utachukua hatua gani baada ya yeye kukiuka matakwa yako. Nilikuwa sahihi mwaka jana na bado niko sahihi leo hii na nitaendelea kuwa sahihi kuwa mapenzi si utumwa wala utwana. Mapenzi ni hiari!
Maana halisi ya ndoa.
Ndoa ni muunganiko wa hiari kati ya mume na mke ambao wamekusudia kuishi pamoja siku zote za maisha yao. Ni muhimu kusema ndoa ni kati
ya mume na mke na sio mume na mume au mke na mke. Katika nchi ambazo wanaruhusu mahusiano ya jinsi moja kisheria, basi mahusiano hayo
huwa hayaitwi ndoa bali 'Civil Partnerships'! Na ni lazima iwe ya hiari! Wanaume ving'ang'anizi mdake hilo.
Section 9.-(l) Marriage means the voluntary union of a man and a woman, intended to last for their joint lives.
Kweli mkuu,
Ila katika hiari hiyo naamini mtu hana ruhusa kusababisha maumivu ya aina yoyote kwa mpenzi wake (to inflict any kind of pains on your spouse). Hapa siongelei kuchapana makonde (corporal punishment)!!
Na kwa sababu hito kifungu cha 64 kinampa mwanamke haki ya kukopa kwa jina la mwanaume (yaani mume atakuja kulipa), kutumia fedha za mumewe au kuuza mali inayohamishika ili kupata pesa kwa ajili ya 'mahitaji yake muhimu' na ya mtoto. Ukimnyima mkeo pesa anaweza kuuza simu yako au hata gari lako ili apate pesa ya chakula au kulipa ada ya mtoto. Ni halali kabisa pale ambapo mume na mke wanaishi pamoja, au wametengana na mume anapaswa aendelee kumtunza au pale ambapo mume amemtelekeza mke
Ni Jukumu la Mwanaume kumtunza mke wake! Maisha yamebadilika siku hizi na wanawake wanatunza wanaume. Lakini sheria yetu ya ndoa katika kifungu cha 63 kinamtaka mwanaume amtunze mke wake kwa kumpatia makazi, makazi, chakula nk. Mwanamke atakuwa na jukumu hilo tuu ikiwa mumewe ni incapacitated na hivyo hawezi kufanya kazi. Mwanaume acha ugumu tunza mkeo otherwise wenzio watakusaidia.
Hapo tupo ukurasa mmoja kaka. Intentional infliction of emotional pain and mental distress is not right whatsoever in any relationship.
Ni Jukumu la Mwanaume kumtunza mke wake! Maisha yamebadilika siku hizi na wanawake wanatunza wanaume. Lakini sheria yetu ya ndoa katika kifungu cha 63 kinamtaka mwanaume amtunze mke wake kwa kumpatia makazi, makazi, chakula nk. Mwanamke atakuwa na jukumu hilo tuu ikiwa mumewe ni incapacitated na hivyo hawezi kufanya kazi. Mwanaume acha ugumu tunza mkeo otherwise wenzio watakusaidia.
Sikubaliani na hicho kipengele. Kinahitaji marekebisho.
Sasa yule demu wako alieyeenda Canada alikuacha mzima kwa hayo maeneo?????
Hayo madhila niliweza kuya pre-empt kabla hata hajafunga hiyo safari yake ya Toronto kwa hiyo nilikuwa pouwa kabisa. Ila nilimaindi kwa muda mfupi.