Mambo muhimu kisheria ununuapo gari

Benbella

Member
Joined
Jul 7, 2012
Posts
11
Reaction score
0
Habari zenu wana Jf, naomba msaada wenu kunijulisha ni mambo gani ya msingi ya kisheria kuyafanya unapotaka kununua gari kwa mtu binafsi yaani gari lake analolitumia au unapoenda showroom hasa jinsi ya kulipana pesa, mashahidi wa kuwatumia, uthibitisho kama gari si ya wizi (hasa unaponunua kwa mtu binafsi), jinsi ya kumbana kama gari litakusumbua baada ya siku chache, jinsi ya kubadirisha jina la umiliki, kujua blue kadi feki au original na mengineyo ambayo mnaona yatanisaidai maana ni mgeni ktk ulingo huu wa kumiliki hivi vitu nisije nikaingia kichwakichwa

Kazi njema
 
Wana JF nasubiria ushauri wenu please, ntawashukuru sana kwa ushauri wenu
 
na uwe macho ndugu yangu.....kuuziwa gari la wizi au lililoshiriki ujambazi ni nje nje......
kama utahitaji ushauri zaidi niPM....
 
na uwe macho ndugu yangu.....kuuziwa gari la wizi au lililoshiriki ujambazi ni nje nje......
kama utahitaji ushauri zaidi niPM....

nashukuru sana kwa hilo angalizo, nipate kwenye bendashy@gmail.com, naweza kukutafuta hata kwa simu, nipate ushauri mzuri zaidi
 
Kama unanunua kwa mtu binafsi, mwambie akupe copy ya kadi ya gari uende TRA. Hapo utapata details muhimu kuhusu umilki halali wa gari husika. Kama ni show room utaoneshwa nyaraka zote zilizotumika kuileta hiyo gari na ukilipa cash siyo mbaya maana utapewa risiti ingawa mimi kwa malipo makubwa kama hayo hupendelea tulipane kupitia bank account. Kama huna haraka sana angiza gari moja kwa moja toka japan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…