Mambo muhimu kuzingatia katika uchaguzi wa kozi chuo kikuu

Maganga Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
2,089
Reaction score
829
Habari zenu. Hongereni wale mliofaulu ...nina vitu muhimu vya kushiriki na nyie siku ya leo hasa kwa kwenye uchaguzi wa kozi vyuoni.

1. Jitahidi kupata taarifa sahihi za kozi unayo/unazotaka kuomba kwa kadiri ya uwezo wako..

2. Usipende kufuata mkumbo; kumbuka hii ni hatua muhimu sana kufikia safari yako ya maisha..

3. Soma vyema sana hiki kitabu - Admission guide book ya mwaka 2014 2015 (nimeambatanisha chini).

4. Kwa wale ambao wanahitaji MKOPO zingatieni sana kozi zenye vipaumbele ...

5. Jitahidi kujua taarifa hizi

a. Important dates to be adhered to during the application process;

b. Minimum entry requirements for each programme;

c. Maximum loanable amount for priority programmes (For more information on Loans refer to issuance of Loans Guidelines and Criteria for academic year 2014/2015 issued by HESLB)

Nawatakia uchaguzi mwema wa kozi..

View attachment Undergraduate Admission Guidebook 2014-2015_04_24.pdf
 
sure..

Kama ndoto yako ni kuwa accountant, kwa mfano, na umefaulu vizuri, chagua kozi za accoutancy tu hata kama ni vyuo mbalimbali.

Kwakuwa TCU wanataka ujaze kozi nyingi, usijaze kozi zisizokuhusu kwa kigezo cha kujaza zile nafasi, utaishia kusoma hospitality management.

Mfano, unakuta mtu anataka kusoma b.com, lakini anajaza education, insurance, heritage.. utajikuta umechaguliwa hizo option nyingine na dream yako unaiaga kiana.
 

Hospitality management ndio kozi gani?
 
Nyongeza:

Ni Hivi kama ile kizo ambayo umeipa kipaumbele cha kwanza kwa bahati mbaya umekosa system haitaangalia tena ufaulu wako mzuri katika chagua lako la pili bali linakuchukulia sawa na wanafunzi wengne katika hilo chagua lao la pili.

Kwa hyo cha muhimu hyo kozi yako ya kwanza uwe una uhakika asilimia zaidi ya 90 kwamba utachaguliwa.
 
Mmm kazi ipo.

Sasa kam dream yko ni kuwa mtu flani na coz unayotaka ili utimize ndoto zako ni non priority. Sasa utafanjaje wakuu?

Niwe radhi kuitosa ndoto yngu au nijaze tu hivyo hivo? Msaada kwa hilo wakuu.
 
Jaza hivyohivyo kama unajua ukikosa mkopo utaweza kujilipia ada na matumizi mengineyo
Mmm kazi ipo.. Sasa kam dream yko ni kuwa mtu flani na coz unayotaka ili utimize ndoto zako ni non priority. Sasa utafanjaje wakuu? Niwe radhi kuitosa ndoto yngu au nijaze tu hivyo hivo? Msaada kwa hilo wakuu.
 
za asubuhi wakubwa!!naomba mnisaidie kuhusiana na kozi za economics ambazo zina market na mkopo ful.
 
7. Usiwe muoga wa maisha kwa kuchagua kozi zenye ajira za serikali tu jaribu hata zile zinazoweza kukufanya ujiajiri. ( maisha hayana specific formula,....... mafungu saba)
 

Mkuu Young mesult sijaelewa vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Mmm kazi ipo.. Sasa kam dream yko ni kuwa mtu flani na coz unayotaka ili utimize ndoto zako ni non priority. Sasa utafanjaje wakuu? Niwe radhi kuitosa ndoto yngu au nijaze tu hivyo hivo? Msaada kwa hilo wakuu.



Usikalili labda kama huna bahati. Mwenzako nilichagua LLB ambayo ni non priority na mkopo nimepata so kama una bahati kama mimi just follow your dream but kama unahisi huna bahati just think otherwise.
 
Usikalili labda kama huna bahati. Mwenzako nilichagua LLB ambayo ni non priority na mkopo nimepata

Mkuu Malengo Jr hiyo LLB vipi soko lake la ajira? Pia naskia ni ngumu sana tena ni miaka 5 kuisoma! Ya kweli haya au ni maneno tu ya kwenye migahawa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Malengo Jr hiyo LLB vipi soko lake la ajira? Pia naskia ni ngumu sana tena ni miaka 5 kuisoma! Ya kweli haya au ni maneno tu ya kwenye migahawa?



Mtaka cha uvunguni sharti ainame pia kipenda roho hula nyama mbichi. Soko la uhakika la LLB mpaka uhitimu law school huo mwaka wa 5 and am ready for that.
 
Last edited by a moderator:
Usikalili labda kama huna bahati. Mwenzako nilichagua LLB ambayo ni non priority na mkopo nimepata so kama una bahati kama mimi just follow your dream but kama unahisi huna bahati just think otherwise.

Ok mkuu nafata ndoto zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…