SoC04 Mambo muhimu ya kufanya ili kukuza sekta ya utalii

SoC04 Mambo muhimu ya kufanya ili kukuza sekta ya utalii

Tanzania Tuitakayo competition threads

shedy22

Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
6
Reaction score
0
Utalii, ni kitendo cha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa lengo la kujiburudisha au kujifunza. Tanzania ni moja kati ya nchi zenye vivutio vingi vya Utalii duniani na ikiwa ni nchi ya tatu barani Afrika kwa nchi zenye Utalii mkubwa. Pia Utalii nchini Tanzania umekuwa na faida nyingi kwa Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na kutoa ajira, uboreshwaji wa miundombinu, kuongeza kipato cha taifa, kuleta fedha za kigeni na kutangaza utamaduni wetu kama Watanzania.

Pamoja na faida zote, sekta ya Utalii nchini mwetu imekua ni sekta inayosuasua kwa kuwepo kwa idadi ndogo ya watalii kutoka nje kwa baadhi ya misimu (Low season) na wakati Tanzania hatujawahi kuwa na joto kubwa sana au baridi kubwa sana kama nchi nyingine zikiwepo za magharibi, na pia Tanzania ni nchi kubwa katika utalii na inaweza kulenga (target) watalii wengi hata Zaidi ya watalii million 10 kwa mwaka wakati kwa sasa tunalenga watalii million tano tu kwa mwaka mzima. hivyo ni lazima Tanzania tujitathmini wenyewe na kufanya mabadiliko ili kukuza sekta ya utalii.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kufanya bayana na jitihada za Mheshimiwa Raisi SAMIA SULUHU HASSAN ili kuweza kukuza sekta ya utalii.

Kuboresha sekta ya Afya. Huduma hafifu za afya ni moja ya sababu zinazopunguza idadi ya watalii nchini. Kwa mfano, kwa sasa watalii kutoka nje wanaofika Serengeti wanapata huduma ya afya kutoka Nairobi- Kenya kwasababu Tanzania hatuna Hospitali yenye hadhi ya Nyota tano (FIVE STARS) kwa kuhudumia wageni wa heshima kama watalii. Kwasababu hiyo watalii wanaokuja wanapata hofu ya kurudi tena hivyo idadi ya watalii kupungua kwa baadhi ya misimu. Kwahiyo, serikali kushirikana na wadau wa utalii wajitahidi katika Kuboresha huduma za kiafya kwa kujenga Hospitali yenye hadhi ya Nyota tano.

Kuboresha miundombinu. Miundombinu kama vile barabara ni muhimu sana katika sekta ya utalii, kwasasa barabara zetu ni mbovu sana kiasi cha kuumiza watalii wakati wa safari kuelekea katika vituo vya utalii, ikiwa ni pamoja na kuwachosha sana watalii, hiyo sababu pia hupelekea kupunguza idadi ya watalii kwa baadhi ya misimu. Hivyo serikali ijitahidi katika Kuboresha miundombinu ya usafiri ili kukuza sekta ya utalii.

Kuongeza ubora wa huduma kwa kuelimisha waongoza utalii. Tanzania inaweza kupokea watalii wengi Zaidi ya tunvyopokea sasa ikiwa tutaelimisha waongoza utalii wetu (Tour guiders) kitu ambacho kitawaongezea ujuzi zaidi katika kufanya shughuli zao kwa ufanisi. Na ninapendekeza kuwepo na sheria ambayo itaruhusu waongoza utalii kwenda kujifunza namna ya kufanya majukumu yao kutoka nchi nyingine zenye utalii kama Afrika Kusini. Kupitia hili tutaongeza ubora wa huduma katika utalii na kufanya watalii kutoka nje kupenda Zaidi kutalii Tanzania hivyo kuongeza idadi ya watalii na kuachana na kesi ya msimu wa udogo (low season).

Kuongeza ubunifu katika Kuongeza na kuboresha vivutio vya utalii. Pamoja na kuwa Tanzania kuna vivutio vingi vya utalii lakini ubunifu katika Kuboresha vivutio hivyo bado uko chini, yaani vivutio vya utalii tulivyonavyo sasa ni vilevile tulivyokuwa navyo miaka nenda rudi, hivyo ni lazima tuwe wabunifu katika kuboresha vivutio vya utalii ili kuingia katika mashindano (competition) na nchi nyinginezo katika utalii, hii ni kwasababu watalii wetu kila wanapokuja wanatukuta na vivutio vilevile hakuna tulichoboresha wala kuongeza inawafanya wasipate hamu ya kurudi tena mara nyingine kwa kujihisi wamemaliza kutalii Tanzania hivyo hupelekea kupungua kwa idadi ya watalii katika misimu tofautitofauti.

Kuanzisha kampeni inayopinga msimu wa udogo (low season) katika utalii. Kwa mfano kampeni inaweza ikawa “HAKUNA MSIMU WA UDOGO KATIKA UTALII TANZANIA” (NO LOW SEASON IN TANZANIA), kampeni hii itasaidia kuweka umakini katika kutokomeza msimu wa udogo katika utalii nchini Tanzania.na hivyo mambo mengi mazuri yatafanyika ili kuitimiliza kampeni hiyo, na hivyo kupelekea msimu wa juu katika utalii (high season) nchini Tanzania kwa kila mwaka hata kupelekea wizara ya utalii kulenga watalii wengi zaidi ya sasa kwa mwaka.

Hivyo basi,
kwakuwa utalii ni sekta muhimu katika maendeleo ya jamii ni lazima serikali yetu ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa utalii nchini, kufanya kila jitihada ili kuweza kuinua utalii nchini mwetu na kufuta kabisa suala la msimu wa udogo (low season) katika utalii kwasababu kwa Tanzania chanzo cha msimu wa udogo (low season) katika utalii sio hali ya hewa wala tabia nchi bali ni ubovu wa huduma zinazotolewa. Pia kwa miaka ijayo Wizara ya utalii itegemee kulenga (target) watalii wengi zaidi ya sasa kwa mwaka ikiwa mambo hayo tajwa hapo juu yatazingatiwa.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom