Mambo muhimu ya kufanya kabla ya kuanza biashara

Travis Walker

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
323
Reaction score
334
Sisi vijana mara nyingi tunapoanza pirika za kutafuta maisha hujikuta tunaingia katika biashara kutokana na msukumo au uhamasishaji wa marafiki ,jamaa ama ndugu zetu ambao wametangulia katika ufanyaji biashara.

Lakini huwa hatukumbuki kwamba biashara inahitaji elimu na kujipanga. Kutokana na sababu hizi basi husababisha kongamano la vijana kufeli katika ulimwengu wa biashara.

01. USIKATE TAMAA BALI SUBIRI.

Kabla hujaanza biashara nakujuza na ya kwamba katika biashara kuna changamoto nyingi mno kama ilivyo katika shughuli nyengine. Changamoto ambazo hutufanya kukosa hamu ya kuendelea na biashara.

Muda huo katika hali kama hiyo hujikuta nyoyo zetu zinakata tamaa na kutamani kuachana na biashara ila muda huo ndio muda wa kufanya subira kwani kipindi cha kupata changamoto huwa ni kifupi sana lakini ni vigumu kufaulu.

02. KUCHAGUA BIASHARA SAHIHI

Mwanadamu amepewa akili na nguvu ili kujiongoza yeye mwenyewe katika maisha. Kabla ya kutamani kufanya biashara chagua biashara sahihi. Kila mtu amezaliwa na kipaji chake hivyo peleleza ni kitu gani unakipenda kutoka moyoni mwako ambacho pia unafikiri unaweza kukifanya.

Kwa mfano mtu akiwa na kipaji cha kucheza mpira basi huyo bila ya shaka anapenda kucheza mpira kutoka moyoni mwake na kama hapendi basi sio kipaji chake. Hivyo ni lazima kwake kukifanyia kazi kipaji chake ili afike kwenye kilele cha mafanikio. Wala usidharau kipaji chako baada ya kujitambua hata kama ni mkulima ila tumia akili kuona ni jinsi gani unaweza kukuza kipaji chako ili kufikia mafanikio zaidi.

Hivyo biashara sahihi ni kufanya kazi ambayo unaipenda halafu una elimu nayo.Sababu watu wengi wanafeli kwasababu ya kuingia katika biashara ambazo haziendani na wao.

03. KUJIAMINI KATIKA BIASHARA

Unapoamua kufanya biashara kabla hujafanya jisemee mwenyeo ya kwamba hutomuogopa mtu na kutokata kufanya biashara hiyo. Kama ukiona biashara yako ni ngumu basi tambua hakuna ugumu katika biashara ila huna wateja hivyo fikiria kutafuta sehemu nyengine ambayo unahisi biashara yako itaendana na sehemu hiyo. Kujiamini ni kuondoa woga na kudumu katika biashara yako.

04. USIOGOPE KUSHINDWA.

Kabla hujafanya biashara,tambua kufeli si kitu kigeni ila usiogope kwani kufeli ni njia moja ya kufanikiwa unajuwa kwa nini nikasema hivyo angalia mchoro uliopo chini utafahamu



Nadhani umeona vizuri mchoro huu . Mchoro huu unaonesha ya kwamba huwezi kufanikiwa mpaka ufeli. Na ndio maana tukasema kufeli ndio njia ya kufanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…