Mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji kufanikiwa

Mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji kufanikiwa

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Wengi wetu mara nyingi huwa tunafikiri kukosa mafanikio ni matokeo ya kukosa bahati katika maisha. Fikra hizo mara nyingi, huwazuia wengi katika kufanikiwa na kujikuta wakiishia kuwa watu wa kulaumu na kushindwa kila siku.

Kimsingi kitu kikubwa kinachochangia kuzuia mafanikio yetu ni baadhi ya tabia tulizo nazo. Si kweli kwamba watu wengi hushindwa kuendelea kutokana na kukosa mitaji bali ni kwa sababu ya tabia zao.

Tabia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya mtu binafsi kuliko unavyodhani.

Zingatia haya yafuatayo ikiwa unahitaji kufanikiwa katika maisha yako:-

Epuka kufikiria sana juu ya makosa uliyoyafanya
Kama kuna sehemu ulikosea katika siku za nyuma, hiyo imeshapita chukua hatu za kusonga mbele. Acha kutumia muda wako mwingi na kufikiri pale ulipokosea kwani hiyo haitakusaidia zaidi ya kukurudisha nyuma.

Kumbuka kuwa kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu, kitu cha msingi jifunze kutokana na hayo makosa.

Usiwe mtu wa kuongelea ndoto zako kila siku
Wengi wetu tumekuwa ni hodari wa kuzungumza juu ya ndoto zetu, lakini sio watendaji. Kumbuka kuwa kama ni kuongea umeshaongea sana juu ya ndoto zako, umefika sasa wakati wa kutenda.

Jenga tabia ya kuchukua hatua dhidi ya ndoto zako kila siku, hata kama ikiwa ni kwa kidogo kidogo ni lazima utasogea tu, mwisho utajikuta unafanikisha kile unachokitaka.

Usisubiri sana kutekeleza ndoto zako
Kumbuka hakuna muda sahihi ambao upo wa kuanza kutekeleza ndoto zako kama unavyofikiria. Muda wa mafanikio na kufanya ndoto zako kuwa za kweli ni sasa na wala si kesho. Acha kuwa na tabia au fikra za kufikiri kuwa mipango yako mingi utaifanya siku nyingine. Anza kutekeleza mipango na malengo yako iliyojiwekea mara moja.

Tumia pesa zako vizuri

Watu wengi huwa ni watumiaji wabaya wa pesa zao, lakini ni vyema ifahamike kwamba matumizi mabaya ya pesa, ni moja ya tabia kama tabia zingine, lakini ambayo ina nafasi kubwa ya kukukwamisha kwa kiasi kikubwa katika kufikia ndoto na malengo yako uliyojiwekea.

Hivyo ili uweze kusonga mbele na kuachana na majuto uliyonayo jifunze kutunza pesa zako vizuri, utafanikiwa.

Epuka kuahirisha ahirisha mambo
Ikiwa kuna jambo ulipaswa kulifanya leo, basi ni vizuri ukalifanya kuliacha na kutegemea utafanya kesho. Wakati wa kubadilisha maisha yako ni sasa na wala si kesho kama unavyofikiri.

Jiulize ni mara ngapi umesema utafanya kitu fulani kesho na hukufanya? Elewa kwamba tabia hiyo ni mbaya na itakuchelewesha sana kufanikiwa katika maisha.

Anza kujiwekea akiba
Ikiwa huwa unashindwa kujiwekea akiba katika kipato katika pesa unayoipata basi jua kitakachokutokea katika maisha yako ni kushindwa kumudu kupata pesa ya kuendeshea miradi yako na mwisho wa siku utakuwa ni mtu wa kulalamika tu.

Kama unataka kuwa tajiri na kuwa huru kifedha anza kujifunza kujiwekea akiba, hii itakusaidia sana kusonga mbele katika mambo yako mengi.

Tambua ya kuwa mabadiliko yako yanategemea sana tabia yako ya kimaisha
Hivyo anza kujiandaa kubadilika wewe kwanza ikiwa ni pamoja na kubadili hizo tabia ulizonazo ambazo zinakukwamisha sana. Kwa kadiri, utakavyoweza kumudu kubadili tabia zako kwa kiasi kikubwa, ndivyo utakavyo jikuta maisha yako yanakuwa na mafanikio makubwa kuliko unavyofikiri.
 
Unapoongelea swala la kuweka akiba zingatia na kipato chako unafanya kazi gani!

Machinga wa mtaani kuweka akiba aisee labda kama una biashara kubwa
Vinginevyo mmm kasheshee
 
Unapoongelea swala la kuweka akiba zingatia na kipato chako unafanyakazi gani!
Machinga wa mtaani kuweka akiba aisee labda kama una biashara kubwa
Vinginevyo mmm kasheshee
Mtu naingiza buku 10 kaa siku hapo hapo bado kula na matumizi kibao. Hafu unasemea akiba.
 
Unapoongelea swala la kuweka akiba zingatia na kipato chako unafanyakazi gani!
Machinga wa mtaani kuweka akiba aisee labda kama una biashara kubwa
Vinginevyo mmm kasheshee
Umeanza vizuri kwamba unapoweka akiba zingatia na kipato chako, lakini baadae unaharibu kwa kutuaminisha kwamba mwenye kipato kidogo hapaswi kuweka akiba, kama huna mazoea ya kuweka akiba hata kipato chako kikikua hautaweka kwa sababu na matumizi yako yataongezeka na hivyo utaona bado kipato chako ni kidogo.
 
Nakubaliana na wewe.
 
Mtu naingiza buku 10 kaa siku hapo hapo bado kula na matumizi kibao. Hafu unasemea akiba.

Mtu naingiza buku 10 kaa siku hapo hapo bado kula na matumizi kibao. Hafu unasemea akiba.
Huu mziki ujue sio kila siku itakuwa hivi
Siku nyingine zinapita patupu
Niambie hapo Akiba inawezekana
Yawezekana na kukosa ulishakopa ili uweze kusonga bila hivyo mm mi simoo
 
Hakika Maisha yana Changamoto zake
Kama kuna mtu aliwahi kutajirika na akafirisika unafikiri tatizo lilikuwa ninii?
Alikosa kuweka akiba?
Alikosa Akili?
Au alipatwa na nini?

Ukipata jibu la hayo nilouliza basi elewa sio kuwa kuwa tajiri kwamba una akili sana au unajua kutafuta kuliko wengine
Hayo mambo sikwambii zaidi yako nje ya Uwezo wangu
Najua unaelewa yako juu ya nani
 
Yanayomkuta Ndg yangu Polepo, au yatakayomkuta yapo nje ya uwezo w...

Hapo kama mwelewa huitaji Shulee

Majibu unayo mwenyewe
 
Mafanikio aya formula namna iyo. Mafanikio huja unapozalisha ziada na ziada
 
Maisha hayana formula hizi mbinu nyingi ni kwaajili ya wale tusio na kipato Cha uhakika, Wenye uhakika wanatumia pesa hovyo sana... Na hawana umakini kama wenye kipato Cha chini... Mwisho wa siku tunabaki na Ile kauli ya mwenye nacho huongezewa.
 
Umesahau kusema ulianza na kijiko sasa hivi unamiliki hoteli..
 
Umeanza vizuri kwamba unapoweka akiba zingatia na kipato chako, lakini baadae unaharibu kwa kutuaminisha kwamba mwenye kipato kidogo hapaswi kuweka akiba, kama huna mazoea ya kuweka akiba hata kipato chako kikikua hautaweka kwa sababu na matumizi yako yataongezeka na hivyo utaona bado kipato chako ni kidogo.
Mafanikio ya kwenye maandishi na mafanikio halisi ni vitu viwili tofauti
 
Wewee
Maisha ya Kiumbe chochote kile formula yake anayo Muumba wetu pekee
Sio kwa Ujanja wa Kiumbe chochote walaaa
Na ukitaka kubisha kuhusu hilo jiulize swali moja
Hivi hakuna watu waliwahi kumiliki pesa zaidi ya Bilion na sasa hawanaa?
Ukibisha kuhusu hilo jiulize je? Mafisadi waliochota pesa kibao hata miaka kumi haijaisha wamebaki kawaida hawapoo?

Ndio ujue maisha ya Kiumbe chochote kile yako kwa Muumba wake sio kwa Ujanja wake
Lijue hilo l
 
Back
Top Bottom