Mambo muhimu ya kuzingatia unapomualika mpenzi nyumbani kwa first dinner date

Mambo muhimu ya kuzingatia unapomualika mpenzi nyumbani kwa first dinner date

iranna

Senior Member
Joined
Aug 4, 2021
Posts
149
Reaction score
621
Mpaka unaamua kumkaribisha nyumbani first dinner mpenzi wako ni lazima umemuamini na kuna vitu vimekuvutia kwake. Hii ni nafasi yako ya kujionyesha kwake uhalisia wako.

1. Nyumba iwe kwenye mpangilio mzuri. Hata kama unaishi kwenye chumba kimoja, tandika kitanda na uandae sehemu za kukaa. Viatu na makololo yawe kwenye mpangilio. (Kumbuka umaridadi huficha umasikini).

2. Usifanye surprise unaweza kuku surprise wewe mwenyewe, muulize vyakula anavyopenda kula kwa ujanja. Andaa vile na wewe unavyopenda kula. Kama mnakula kwa mikono maji na basin la kunawia viandae mapema.

3. Usichanye glass, hata kama hujui kabisa goole picha za juice glass, beer glass, wine glass, weka vinywaji kwenye glass zake si kuweka wine kwenye juice glass.

Kwa heshima mpe mgeni nafasi ya kuanza kupakua chakula, mziki wa ala wa sauti ndogo huwa unapendeza wakati wa chakula.

Usipende kuongea na chakula mdomo ni, maongezi yawe mafupi wakati wa chakula ikiwezekana kujibu maswali. Unaweza kupaliwa hamu ya chakula ikaisha.

Baada ya chakula weka matunda kama mgeni ana nafasi ya muda na maongezi yataendelea.
 
Mie hayo ya kuigiza yameshanishinda..

Kama sijatandika kitanda na anakuja ajege tu, sijisumbui kutandika.. Anione mimi halisi akinielewa sawa, akishindwa basi, mapenzi ni kujuana na mapungufu yenu, kisha mmoja akkaziba pengo kwa mapungufu yale.
 
Kwa mimi dinner sileti demu ghetto, kazi yangu moja kujua anapenda nini, na kwa wakati huo pesa anayo au hana na anatamani nini basi, na namwambia in advance kuhusu dinner ila navuta kama mwezi huku naona nae na hello za hapa na pale na lunch kimtindo simple tu na style flani ya nywele nikiipenda nauliza bei yake siku mmoja namshangaza namgea namwambia kesho nafsi yangu itafarijika ntahisi kutoa chozi nikuone umesuka ile style yxyjojo
 
Back
Top Bottom