Mambo muhimu yakufanya katika biashara yako

Joined
Jan 10, 2015
Posts
78
Reaction score
27
FANYA HAYA UTAFANIKIWA SANA KWENYE BIASHARA

Watu wengi wanaanzisha biashara, watu wachacahe wanafanikiwa kwenye biashara, usishangae unaweza anzisha biashara na usifanikiwe ukaanza kumtafuta mchawi kumbe mchawi ni wewe, hebu tujigunze pamoja mambo ambayo ukiyafanya hata kama unauza nyanya nakuhakikishia mafanikio ndani ya muda mchache.


1.USIPENDE KUONGEA TU TENDA

Unakuwa mfanyabiashara ambae kazi yako ni maneno tu, unataka mafanikio lakini mafanikio yako yako mdomoni, hilo ni tatizo yani kila ukiambiwa kitu unajua, kila kitu lakini katika utendaji ni ziro, katika maisha unapoamua kufanikiwa usipende kuropoka utafanya hichi, we ni mtaalamu wa hiki, na kile wakati umaona bado hujakifanya hata kama una wazo zuri vipi lakini kama hujaliweka kwenye matendo ni kazi bure, jifunze kile ambacho unaona kwako kinafaida kitende tena kitende kwa moyo mmoja.usiogope wala usiangalie nani atakuonaje we tenda halafu baadae watakuuliza hivi hayo mafanikio ndio ile biashara? Unawaambia ndio.


2.JUA KITU GANI NI MALENGO YAKO MAKUBWA

Unapoanza kutafuta mafanikio au unapoanza kufanya biashara hebu usianze biashara kama mdudu hebu usijiulize hivi wateja nitatoa wapi? Hili ni swali la watu wengi sana ambao ni wavivu wa kufikiria yani anaanzisha biashara swali la kwanza anajiuliza wateja nitatoa wapi? Swali la kwanza unalotakiwa kujiliza kwanini nimeamua kufanya biashara, ukijiuliza swali hili utapata makusudi yako maalum ya wewe kufanya hiyo biashara hata kama akija nani kukwambia hiyo biashara haifai, hutaweza kumsikiliza, kwasababu yeye hajui malengo yako.wewe ndio ambae unafaham malengo yako.ni rahisi sana kufanikiwa kama utatambua malenho yako yamsingi, nakumbuka wakati naanza biashara nilikuwa nakutana na challenge nyingi sana lakini kila nilipokuwa natakakuacha moyo ulinisuta na kuniambia umeshatimiza malengo yako? Nakuta bado naendelea.


3.ANZA MWANZO

Usipende kuanzia juu siku zote kwenye maisha yako, usipende kuanza na mataji mkubwa sana hata kama pesa ipo, jifunze kuanzia chini halafu anza kupanda juu, ukianzia chini maisha yako yatabadilika kwasababu utajifunza unajua kinachowafanya watu wengi kufikia kuona biashara ji ngumu wanataka mafanikio ya haraka haraka na wanataka kuanzia na mtaji mkubwa ndio maana mtu anaweza kuwa na milioni moja akakwambia sina mtaji, hee hii yote ni kwasababu anataka kuanza kwa ufahari, ajulikane ameanza na kujaza frame bidhaa, acha tabia hizo.


5.ACHA KUFANYA VITU KWA KUA GALIA WATU

Rafiki hakuna mtu anajua unataka nini kwenye maisha, hata kama uko vipi usifanye kitu kwa kuangalia watu wengine, eti rafiki yangu akiniona nafanya hii atanionaje, je na yule ndugu yangu ananijua me nafanya kazi nzuri akinikuta nauza sabunj atanichukuliaje, hizo ni tabia za kimasikini hakuna mtu yeyote ambae atakuwa na mchango katika maisha yako isipokuwa wewe, acha kuishi maisha ya photocopy, ishi maisha yako halisi, ukiishi wewe kila kitu kitakuwa sawa.lakini ukiishi kwa kuwaangalia walimwengu hutafanya cha maana, maana dunia hii imejaa wakatisha tamaa kibao.

HAKUNA ANAEJUA THAMAN YA MAISHA YAKO ISIPOKUWA WEWE ACHA KULALA MAISHA YANAENDELEA
abtwahil@gmail.com
 
Asante sana Mkuu kwa elimu kuongezea nyama kwenye uzi wako pia suala kubwa linalotakiwa ni kujitambua wewe ni nani na anaweza kufanya nini? wengi wanafeli pia kutokana na kushindwa kujitambua asili yao kama ni ujasiriamali au ni biashara wanaanzisha biashara na mwisho wananishia kufeli sababu ya kuingilia mlango wao wa kutokea.

Mfanyabiashara akikomaa anakuwa mjasiriamali, na Mjasiriamali akikomaa anakuwa mfanyabiashara lakini wote ni lazima waanzie kwenye asili yao.
 
Mkuu sijaona suala la IMANI kiongozi inategemea na vile anavyoamini mhusika.

Wengine humtanguliza MUNGU ili mambo yaende sawa na wengine hupitia sehem sehem ili kuweka mambo sawa na kuondoa uzito kwenye BIASHARA KIONGOZI.

AU UMESAHAU KUWA BIASHARA IMANI...?
 
Mkuu ninataka kuanza biashara ni gradaute engineer na maisha magumu sana mtaani nina laki moja mkononi ebu nishauri mkuu nifanyeje na hyo laki moja ili maisha yasonge,maana nashindwa kuamua
 
Mkuu ninataka kuanza biashara ni gradaute engineer na maisha magumu sana mtaani nina laki moja mkononi ebu nishauri mkuu nifanyeje na hyo laki moja ili maisha yasonge,maana nashindwa kuamua

daa kijana mwenyewe graduet kma wewe nimefungua genge huku bunju nilianza na ef 50 nikawa nafunga ndiz ilikuwa wa 10 leo ninagenge la kma lak 6 hv!!usione aibu kwa mtu sabb ni graduet hamna mtu anaekusaidia anza tu kaka!!
 
Daah pamoja sana mkuu ngoja nichukue ushauri wako niufanyie kazi hakuna kuona aibu.tutatoka tu mwisho wa siku
 
poa sana mkuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…