Uchaguzi 2020 Mambo muhimu yanayokifanya Chama cha Mapinduzi kiweze kuibuka kinara katika uchaguzi 2020 Oktoba 28

Uchaguzi 2020 Mambo muhimu yanayokifanya Chama cha Mapinduzi kiweze kuibuka kinara katika uchaguzi 2020 Oktoba 28

Kijana ushe2

Senior Member
Joined
Apr 6, 2017
Posts
179
Reaction score
127
Imeandaliwa na Mwl.ngh'oloyape,

Habarini wanajamvi wa siasa forum nimejaribu kufuatilia siasa za Tanzania na jinsi ambapo tunajinasibisha mitaani kwamba Lissu atakuwa Rais wa JMT nimegundua na kuweza kuona hawezi kufikisha 40% kwa ujumla katika uchaguzi huu kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Chama cha CCM kina wapiga kura wao wanaojulikana kati ya hao watakaokeng'euka ni wachache wengi watamchagulia Mwamba JPM bila kupepesa macho kiuhalisia.

2. Lugha za kutishana za Lissu zinamtolea kura kwa watu wa vijijini na wale wanaomheshimu kwa kauli hizo tayari wanaona huyu sio Rais anayetufaa anataka kutumia mabavu kabisa walakini

3. Siasa za CCM zinaanzia shina na familia hivyo basi wanaweza wakashawishi kuwachukua wananvhi wasio na chama wakakipigia chama hiki kikuu na tawala nchini(HII NI TURUFU INAYOWAFANYA WAFANIKIWE SANA KATIKA UVHAGUZI MAANA VIONGOZI WA MASHINA NDIO HUFANYA SIASA KUBWA NA KALI MNO NA ZENYE MUONEKANO WA KURA ZA MOJA KWA MOJA BILA NINI ) hii nina uzoefu nayo kwa asilimia 100% maana nimeweza kushiriki katika kuona na kuoneshwa namna gani kura huwa zinatafutwa kabisa

4. Mahaba na JPM yamezidi mno kwa wananchi na sio wakereketwa hawa ndio wanamdanganya TUNDULISSU hapa sio ubunge ni urais kuna sehemu unaweza ukajaza ukafikiri ndio kura hizo kumbe sio kura wale ni vijana ambao wanaweza kuja kukuangalia kukuona TUNDULISSU huwa yukoje?anaongeaje? Na wengine wanakuja kuangalia hivi huyu atajaza? umbe ndio wanajaza hivohivo wao bila kujua lakini wengine wanataka chochote hapohapo kwenye kampeni.

5. Wafanyabiashara hawapigi kura na wasomi wengi sio wapiga kura hivo basi ni vigumu sana kumshinda mtu ambae ana mizizi mingi Tanzania nzima kaweka mgombea ubunge na udiwani umshinde hiyo ni ngumu mno.

Nasubiria povu narudi kwetu kijijini USHETU ELIUS JOHN KWANDIKWA chapa kazi mheshimiwa tunakutegemea wewe una MISSION VISION NA GOALS Tunampenda sana mbunge wetu.

MAGUFULI MITANO TENA
 
Lugha za kutishana za Lissu zinamtolea kura kwa watu wa vijijini na wale wanaomheshimu kwa kauli hizo tayari wanaona huyu sio Rais anayetufaa anataka kutumia mabavu kabisa walakini
Kama ni kutisha hakuna anayemzidi Magufuli. Watu wamepata masfa, rambirambi zimetolewa halafu akula?

Anabomolea watu majumba yao halafu anawaacha bila fidia? Wakati mahakama imeamua walipwe.
 
Kichwa

Lissu the greatest

Screenshot_20201018-111458_1603115382434.jpg
 
Mbona huwa mnakariri vibaya hivi?
Hizo shule mnazosoma ni za kazi gani?
Hiyo point namba 5 imekuabisha sana
 
Kwa hiyo mnawasifu CCM kwa Kuondoa FAO la kujitoa?

Ndugai na Magufuli wakaleta Sheria mwaka 2018 ya Kuondoa FAO la kujitoa?

Bureau De Change...mkapora fedha za watu.

Arusha na Moshi wanamsubiri Magufuli aje kujibu hayo.

TRA kufilisi watu

Msilete poyoyo za Reli, CCM iliua Reli.
 
Sherehe zimeanza mapemaaa

Binafsi nampa Lissu chance ya 70% kushinda uchaguzi huu. Hii ni kwa sababu kampeni yake imekuwa almost perfect. Ameepuka makosa yoyote makubwa ya kiufundi na amejua mbinu sahihi za kuyaongelea makundi mbalimbali ya wapiga kura.

Nimempa Magufuli 30% chance kwa sababu kwanza inabidi umpe heshima mpinzani wako na bado vile vile anashikilia mpini kwa hiyo hizo ni percentage za heshima kwa nafasi aliyo nayo sasa hivi. Ila uchaguzi huu anakwenda kushindwa!
 
Huu mwaka CCM kupitia kile kijamaa kinaitwa Polepole sijui , mmeamua kuongea ukweli toka mioyoni kwa kukubali kuwa nyie hampo kwa ajili ya wananchi maskini.

Kamwe hamjawahi kuwa. Zaidi ni kwamba mnastahili kuondoka madarani. Mmekula mmevimbiwa, hamna UTU. Hadharani mnawatweza walalahoi walipakodi mnazofuja!
 
Aiseee yamekuwa haya tena? Hakuna cha flyovers wala SGR? Wapiga debe mnamharibia mgombea wenu sana tu.
 
Back
Top Bottom