Dr Chi
Member
- Dec 20, 2016
- 15
- 16
1. FANYA TAFITI NDOGO KUWAHUSU.
Muulize mwenza wako kuhusu asili yao, namna wanavyoishi, nini unatakiwa ufanye na nini hutakiwi kufanya.
Jifunze kusalimia kwa lugha yao kama sio ngumu sana, watafurahi kuona unajitahidi kuwa kama wao na hii itaonyesha ni kwa namna gani upo serious katika kujenga familia na mtoto wao.
Jifunze kuhusu vyakula wanavyopenda na hata jinsi wanavyokula. Usiende ukweni ukiwa hujui lolote kuhusu wao, maana kile wanachokiona kwako kwa mara ya kwanza ndicho watakachobaki nacho.
2. VAA VIZURI.
Kwa binti vaa nguo za heshima, vaa nguo za heshima kwa mtazamo wao na sio wako. Inawezekana kabisa katika jamii uliyokulia kuvaa nguo fulani sio shida ila inawezekana pia nguo hiyo kwa jamii ya wakwe zako sio ya heshima, elewa hilo.
3. USIENDE BILA ZAWADI.
Usiende bila zawadi, unaweza kuona sio kitu muhimu ila kinatengeneza kumbukumbu kubwa sana, hasa kwa mama mkwe na watoto kama wapo.
Hizo kumbukumbu zitabaki nao siku zote, na thamani yako kwao itakuwa kubwa sana.
4. USIWE KARIBU SANA NA MWENZI WAKO.
Unapokuwa ukweni usiwe karibu sana na mwenzi wako, umepelekwa ukawasalimie wakwe zako na ndugu waliopo huko, hao ndio watu uliowafuata.
Epuka muda wote kutaka kuwa na huyo mpenzi wako na ukawa huna muda watu uliowakuta huko, hii haina faida ya wewe kwenda kule. Ambatana na watu uliowakuta na ujichanganye nao katika mazungumzo na shughuri za hapa na pale.
5. PUNGUZA MATUMIZI YA SIMU.
Haileti picha nzuri kwa wenyeji wako wewe kuwa busy na simu yako, tena kwa binti ni mbaya zaidi, kama matumizi yako ya simu ni makubwa sana unapokuwa ukweni unashauriwa utoe mlio na uwe unaiacha chumbani muda mwingi wewe ukiwa nje na wenyeji wako.
6. JICHANGANYE NA WENYEJI WAKO.
Unatakiwa kujichanganya na wenyeji wako, katika mazungumzo na kazi za kila siku. Hii itakusaidia kuwazoea na kuwajua kwa undani na kuwa huru kwao.
7. FANYA WANACHOFANYA.
Kama wanapika pika nao, kama wanaosha vyombo osha nao na shughuri zingine kama hizo.
8. MSIITANE MAJINA YENU YA KIMAHABA UKWENI.
Unapoenda na mmeo au mkeo kwenu, kama mna watoto itaneni baba fulani au mama fulani, sio mbele ya wazazi mnajiita majina yenu ya mahaba sijui baby, sijui sweet, sijui laazizi hapana.