Mambo ni mazito! Marioo ahisi Chino alituma watu wamwekee sumu 'Hii chuki imekuwa kubwa sana'

Mambo ni mazito! Marioo ahisi Chino alituma watu wamwekee sumu 'Hii chuki imekuwa kubwa sana'

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Saga la Marioo na Chino Kid linaendelea kuchukua sura mpya, huku Marioo akielezea hisia zake kuhusu uhusiano wao wa zamani.

Marioo ametaka mashabiki kumuuliza Chino ni wapi alikosea, akisisitiza kuwa alimuonyesha upendo na kumuunga mkono kila wakati.
IMG_0304.jpeg

Marioo anasema amekalia kimya matatizo hayo kwa muda mrefu, lakini anashangaa jinsi Chino anavyoendelea kumzungumzia vibaya kwenye mitandao ya kijamii, licha ya kumsamehe. Hali hii inamfanya Marioo kuhisi kutokueleweka na anashuku kuwa Chino anaweza kuwa na sababu za msingi za kumtaka kuonekana mbaya ili kujitengenezea jina katika tasnia ya muziki.

Katika andiko lake, Marioo anasema: "Ndugu zangu, naomba mnisaidie kumuuliza Chino ni nini nilikosea, ambacho mimi sikijui zaidi ya kumuonyesha upendo na kumsupport. Swala hili nimelikalia kimya muda mrefu, lakini sasa limekuwa kubwa. Mimi pia ni binadamu, kila ninapojitahidi kutengeneza mazingira ya amani, wananiona mimi mnyonge."
IMG_0300.jpeg

Marioo pia ameeleza wasiwasi wake kuhusu chuki anayoiona kutoka kwa Chino, akisema: "Hii chuki imekuwa kubwa sana kiasi kwamba naanza kuamini pengine ni kweli alihusika kutuma watu waniwekee sumu, ambayo namshukuru Mungu tulifanikiwa kuiwahi."
IMG_0299.jpeg
 
Back
Top Bottom