Mambo "Siriasi" yanapogeuzwa vichekesho

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Siku hizi naandikiana sana na vijana na kwa kweli wakati mwingine nausudu staili zao za uandishi.

Nikawasahihisha kwa kuandika, ''nafikaga,'' wananijibu.

''Mzee hebu ''relaksi,'' kidogo kwani hujanielewa?
Hatuko kwenye chumba cha mtihani hapa.''

Nami nawaheshimu hawa vijana kwa kuwa wananisoma sana na waniuliza maswali mengi.

Sasa nafata ule msemo, ''When in Rome do as the Romans do.''

Nishapata homa ya kuogopa kuachwa nyuma.

Sasa nina ''relaksi,'' na hawa rafiki zangu ingawa sijapenda kabisa kuona lugha inakua kwa mtindo huu maana nimemsikia Sheikh Adenanga akisema kuwa neno likitumika sana na kuzoeleka linatiwa katika msamiati na kuwa rasmi.

''Nasomaga'' na ''siriasi.''

Wanigeria wanaongoza kwa kufanya mambo mazito ya uendeshaji serikali yanapokuwa tatizo kwa viongozi wao kuwa vichekesho vyao wakachekeshana.

Uchaguzi wa Zanzibar ile staili ya kuchukua 'Roll Call,'' katika mapokezi ya viongozi, maandamano na kadhalika siku ya pili ungeona kibwenzo katika gazeti kinaonyesha wagonjwa wamekodi lori wako nyuma ya lori wamelala kwenye vitanda vya hospitali na ''drip'' zao zinaning'inia na vyuma vya uzito kwa waliovunjika miguu wako katika maandamano au mikutano.

Au kibonzo kingemuonyesha mkubwa wa ofisi na makaratasi yake kasimama juu ya lori anaweka tiki kwa wagonjwa waliohudhuria.

Wanigeria wanaamini kuwa vibonzo vya kuwananga viongozi vinashusha hamaki zao wanaishia vicheko na vicheko si sawa na kupopoa mawe na kuchoma matairi barabarani na mitaani.

Naona na sisi Tanzania tunawaiga na huenda si muda mrefu tukawapita.

Sipiti kijiwe lazima vijana watanisimamisha ati wanataka kusikia mawazo yangu.

Nimekuta ubishi mkubwa wanabishana kuhusu Nusrat Hanje kutolewa jela.

Mmoja anamwambia wenzake ingekuwa yeye yuko lupango mvua 12 zishanyesha anakula nyuka na dona baridi limevaa koti kisha ghafla anakuja malaika kumtoa jela na anampa kigunia cha noti na kazi ya uhakika angekataa kwenda kuapishwa?

Nyie mna roho mbaya sana nyie mnafurahia matatizo ya wenzenu.

Wewe jela unaijua au unaisikia RTD?''

Nasikia sauti inajibu, ''Wewe CCM nani asiyekujua?''

Nimesimama kama mti wa stimu nasikiliza.

Nyuma yangu mwingine anasema, ''Haya na wale masheikh wa Gwajima vipi wale?''

Jibu linavurimishwa, ''Masheikh wale wana njaa sasa nani atakataa hela ya bure hata jasho hutoki wewe ungepewa ofa ya Gwajima ungeipiga teke mwanangu?

Unakunja mkwanja wa maana na unapigwa na suti ya kanzu ndani ya basi full kiyoyozi hadi Dodoma.''

Mwingine anasukuma, ''Nani kakwambia wale masheikh?

Kuvishwa kanzu na kofia na Gwajima ushakuwa sheikh?

Gwajima kawapa full suti wale masheikh kuanzia kofia, kanzu hadi makubadhi.''

Chuma kingine kinavurumishwa kwangu, ''Mzee Mohamed wale si masheikh wa BAKWATA wale?''

Hapa mwili unanisisimka.
Natoa udhuru na vijana wananiruhusu kuondoka.

Nyuma yangu nalisikia zogo bado linaendelea.

Mambo haya hunipa sana mawazo.

Maneno ya hawa vijana yamejaa mengi ya kuweza kujua jamii yetu ikoje.

Hakika hata upuuzi huwa na faida zake.
 
Utanisahihisha maalim pana msemo husema "there is a sense in a nonsense " humaanisha nini?
 
Lugha yeyote Duniani ina uhai!!......Kwa maana kuwa inazaliwa, inakua, inaishi na inakufa!! mfano Lugha ya kiyahudi cha kale aliyo itumia Yesu kimekufa kifooo!! ivo nakushauri achana na lugha ya kizamani mzee!.....ukisikia Neno km ,

Nyomi,

oyaa! inakuwaje Masera wangu!

Hakuna wa kuzuia moto huu!! Mchere! mchere!

Gari imekula shazi!/ nyomi! kituo cha kwanza posta! sijui yange yange kibao!

Daaa! ee! banae Ndinga imeenda shule ile Mwana! si kitoto! siri - cha ''A'' town!! unakijua Mzee? au!

Mtiti!...au niondolee nzi! (kiwingu)...ujue ndo lugha inakua ivooo! Yakupasa uyaelewe/uyakubali haya!

Bush star hapo Babu hawezi nyaka kitu hapo! ni bila! bila tu!..au unasemaje Mkuu Babu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…