Mambo unayopaswa kuyaomba kwenye maisha yako pindi Tu utakapoanza kujitambua!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAMBO AMBAYO UNAPASWA UYAOMBE KATIKA MAISHA YAKO.

Anaandika, Robert Heriel.

Maisha yanaogopesha, yanatisha Kama nini, kila siku mambo yanabadilika, mtunzi wa maisha amefanikiwa katika Kazi yake kuhakikisha hakuna ajuaye hatua hata moja inayofuata, hakuna awezaye kubashiri filamu hii ya kutisha na kusisimua itaishaje na ilianzia wapi. Safari yenye wasafiri wasiojua wapi walikotoka na wapi waendako na lini watafika, wakiwa ndani ya chombo ambacho Dereva wake haonekani. Doooh!

Niite Taikon wa Fasihi, Mwanafalsafa katika chombo; Msafiri kutoka Nyota ya Tibeli.

Labda ningejipa kazi isiyo na faida ningepata hasara kupoteza muda na wakati wangu. Au ningejipa kazi yenye hasara ningepata faida ya kuulinda muda na wakati wangu. Lakini Nani aliyenidanganya kuwa Mimi Taikon Nina muda na wakati wangu kama nalikuja uchi nikiwa sina chochote, tena wala sikumbuki siku Ile Ilikuwaje na nilikuja muda gani, na Nani walinipokea zaidi ya kuambiwa basi sina cha kupoteza, wala sina hasara Kwa maana hakuna kilichochangu.
Nalizaliwa sina kitu na nitakufa sina kitu.
Ndipo nikajua yakuwa Kwenya maisha hakuna faida wala hakuna hasara.

Wala hakuna lolote litakalo hesabika ni faida kwao wataondoka bila ya chochote, na hakuna lolote litakahesabika ni hasara ikiwa Twalikuja tuu uchi.

Safari yetu ilianzia baada ya Mwanzo kupita, tena ikakoma kabla ya mwisho kufika. Huyo Mtunzi na mwanzilishi wa safari hii alikuwako na kabla hajaondoka alituweka naye hakusubiri kumbukumbu zetu zilipoimarika akaondoka bila ya Sisi kumuona, hatumkumbuki! Hatumjui tena! Mpaka kumbukumbu zetu zitakapopotea fikarani, na sauti zetu zitakapotokomea mawazoni, miili yetu itakapotudi mavumbini. Doooh!

Tukaja kila mmoja Kwa taraja lake, lakini Nani aliyetuambia tuna haja na matamanio yetu, labda kama tungejua kusudi la kuwapo hapa safarini tungeweza kusema hivyo.

Kama ningemuona Dereva wa chombo hiki ningemuuliza sehemu ya Yale aliyoyaweka akilini mwangu, lakini kabla sijamuuliza labda ningejiuliza mwenyewe ni vipi nikute maswali Kwa uwazi fikarani naam ndio kichwani mwangu lakini nisijue yalipofichwa majibu mawazoni mwangu.
Maana Kama aliweka maswali katika kichwa changu basi lazima pia aliweka na majibu hata sehemu ya Siri katika ubongo wangu.

Sasa nitamuomba, Yale maswali uliyoyaweka nimeyaona, sasa uniambie yapo wapi majibu ya maswali ulioyaweka? Kama katika kila swali; jibu hufichwa katikati ya swali, na katika kila Fumbo la Siri; jawabu hufichwa chini Kabisa ya fumbo hilo basi nitakuomba unionyeshe jawabu la maisha katika kila njia niipitiayo.

Nitamuomba nisiyemuona! Au je nitawezaje kuwa na matarajio katika safari nisiyoijua mwelekeo wake na Dereva wake. Au pengine niweke mipango kwenye mipango iliyowekwa ikiwa Mimi pia ni sehemu ya mipango ya Mtunzi. Filamu hii inatisha Kama nini, nipo ndani ya simulizi namuambia mtunzi fanya hivi au fanya vile, kisha namueleza nataka hiki au kile, iwe hivi au iwe vile. Huyo mtunzi huenda atashangaa kujikuta yeye ndiye mhusika na Mimi ndiye Mtunzi nikibuni na kutunga visa vyangu mwenyewe vile nionavyo. Lakini vipi Kama Mtunzi alimuumba Mtunzi mwingine ili kujipunguzia kazi ya kutunga visa na simulizi ya Ile filamu yake isiyo na mwisho, Kwa maana yeye Hakuwa na mwanzo wala Hana mwisho lakini wale watunzi wengine, naamn ndio Sisi tutafika mwisho wa utunzi wetu Kama tulivyokuwa na mwanzo WA utunzi wetu. Loooh!

Nitaomba nini ikiwa tayari ni mtunzi mtunzaji wa simulizi iliyotungwa nisiyojua mwisho wake, labda simulizi ilikuwa wazo tuu fikarani mwa mtunzi, nami ni mfano wa kilichopowazoni kikaweka kionekane na kishikike, labda maisha ni video ya kile alichokuwa anakiwaza mtunzi.

Ningemwambia mtunzi nataka niwe mwisho wa Stori yako ili niujue mwanzo wako, hapo angekataa najua, angesema wewe ni udongo tuu wawezaje mwambia mfinyanzi nifanye hivi au vile. Basi sitaomba kitu, hivyo navyo labda nitaonekana kiburi na jeuri. Mtunzi aliweka utunzi fikarani mwangu, yakuwa nimuombe Kama sehemu ya yeye kujiomba mwenyewe. Hahahaha! Kumbe mtunzi anajiomba mwenyewe kupitia watunzi aliowatunga. Doooh! Hii nayo faida yake ni ipi, na Hesabu ya hasara yake ikoje.

Kama mtunzi angeweka makadirio ya wakati na muda katika Kazi yangu, na katika njia zote nitakazopita, akaweka kadiri ya haja na Mapenzi yangu basi yeye angekosa kuwako, kwani watunzi waliotungwa wanahaja na mambo makubwa yaliyowazidi hata yasingewatosha. Hiyo ingehesabika Kama Uovu na uasi Kwa Mtunzi Mkuu.

Katika maisha huwezi omba lolote kwani yote utakayoyaomba ni sehemu yako mwenyewe, yapo katika utunzi wako, mtu hajiombi Kwa Yale alokuwa nayo Ila Kwa Yale asiyokuwa nayo. Lolote lililopo mawazoni na fikarani mwako ni lako. Huwezi liomba isipokuwa unaweza kulitoa mawazoni na kuliweka mbele machoni ili liweze kuonekana katika utunzi wako.
Kama Mtunzi hawezi kuombwa na Wahusika katika filamu yake ndivyo na wewe katika maisha yako huwezi kuomba haja zilizoko katika moyo na akili yako.

Nipumzike sasa!
Ni Yule Mtibeli kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
lakini kabla sijamuuliza labda ningejiuliza mwenyewe ni vipi nikute maswali Kwa uwazi fikarani naam ndio kichwani mwangu lakini nisijue yalipofichwa majibu mawazoni mwangu.
Maana Kama aliweka maswali katika kichwa changu basi lazima pia aliweka na majibu hata sehemu ya Siri katika ubongo wangu.

Sasa nitamuomba, Yale maswali uliyoyaweka nimeyaona, sasa uniambie yapo wapi majibu ya maswali ulioyaweka?
sehemu ya majibu ipo mkuu... tena katika ubongo wako... it is known as pineal gland a.k.a the seat of the soul
 
Leo kwenye kijiwe chenu Cha kahawa huko ndo mlivyochambua kwamba watu hawawezi kumuomba Mungu yaliyo mawazoni mwao......
 
Ukweli kuhusu maisha umefungwa na watu wa dini na wale walio na nguvu fulani katika dunia, wao wanataka dunia iwe hivi au vile hivyo hujaribu kuzuia kwa namna yoyote watu kupata maarifa kuhusu maisha.

Maisha yetu tunaishi hatuwezi kujitenga na wanyama, na pengine aheri wanyama wao wanaenda tu ilimradi mawio na machweo ya jua yanawafikia.

Sisi tunakula kila siku na kushiba lakini haturidhiki, tunafurahi lakini hatutosheki, kila tunachokifanya kimepungua hatuna mbele wala nyuma tupo tu ilimradi tupo.

Kusali tunasali lakini hatufikii tumaini wala tarajio letu, kwa ufupi ukweli kuhusu maisha umefungiwamahali na watu fulani.
 
Kumbe tumaini la kwenye sala ni mali na mafanikio...........
 
hata wewe ukiamua unaweza kuujua ukweli kuhusu maisha mkuu ... unaweza kuwa hao watu fulani
 
Back
Top Bottom