Mambo usiyoyajua kuhusu maombi ya 'Passport'

Mambo usiyoyajua kuhusu maombi ya 'Passport'

steve_shemej

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,175
Reaction score
1,588
Kuna mambo fulani idara ya uhamiaji hawajayaweka sawa

Ukiingia katika tovut ya uhamiaji utakuta kuna vielelezo unavyotakiw kuwa navyo ili upate passport lakini kuna maelezo hawajayaweka vizuri

Mfano:

Kiapo
Wamesema kama huna cheti cha kuzaliwa unatmia kiapo lakin hawajasema kuwa kiapo kina tumiwa na watu waliozaliw mwaka 1980 kurudi nyuma kuanzia mwaka 1981 kuja sasa kiapo hutakiw kutumia.

pia kama kama ulipata chet kupitia mfumo wa rita wa kujaza form mtandaoni pia huwez pata passport kwakuwa vyeti vilivo ombwa mtandaon havina taarifa zote

'Barua ya Mwenyekiti'
Hii haipo kwenye viambatanisho walivyo orodhesha lakin bila barua hati hupati

Wazamini wawili
Hawa hawajaorodheshwa lakini bila hawa hati hupati

Ndugu wawili
Nao hawajaorodheshwa ila bila hawa hati hupati

NB: Vizuri uhamiaji wangekuwa wawazi waweke vigezo na maelezo yote watu waelewe
 
Mambo ni mengi mno , ngoja nifuatilie nione
 
NB: Vizuri uhamiaji wangekuwa wawazi waweke vigezo na maelezo yote watu waelewe.



[emoji115]

Ndiyo maana waafrika tunaendelea kukwama kila uchao. Ukute hivyo vilivyofichwa ni fursa za watu
 
Kwa hapa kwetu ZANZIBAR unapoongeza muda (renew) wa pasi baada ya kumaliza muda wake process yake ni sawa na ya yule anaeomba mpya. Yaani unaanza kuombwa tena vitu vyote ambavyo umewahi kuwasilisha ulipoanza kuomba.

Hili la kuongeza muda linafaa lirekebishwe litafautiane na lile la maombi mepya. Sina hakika kama utaratibu huu ni nchi nzima au ni sisi tu huku.
 
Na hivyo vigezo vikitimia inachua muda gani kutoka hiyo pass
 
Na hivyo vigezo vikitimia inachua muda gani kutoka hiyo pass
Inachukua wiki tatu hadi mwezi na wiki kadhaa kuendana na idadi ya maombi ya wakati huo....hakikisha umeorodhesha kila kitu wanachohitaji ha hata ukiwa na vya ziada inasaidia kama vyeti vya shule n.k
 
Back
Top Bottom