Mambo/vitu ninavoviwaza kwa muda mrefu akilini

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Tuseme hata usiku ukiwa macho Jambo lipo ambalo linakusumbua Sana akili katika aspects mbalimbali na unaliwaza Sana
Mimi katika Mambo ya mahusiano nawazaga Sana kuhusu mchumba wangu flani ninataka awe mke wangu lakini tuko dini tofauti me mkristo inakuwa sana ukizingatia Ana imani Kali Sana kwenye dini yake kila siku najiuliza atakubali kweli nimuoe au nicheki wachumba wengine tu nisipoteze muda bure nikaja kupigwa kibuti dakika za mwishoni

Mimi katika ishu za uchumi na fedha nawazaga Sana kuhusu madeni sugu ninayodai watu hivi kweli nitalipwa au niyasamehe tu nitafute pesa pengine ku replace hela yenyewe ngumu kwenye biashara nawazaga kila siku lini nitaitwa kwenye ajira nimechoka kudai watu karibia mia.nikilala usiku natamani lolote litokee serikalini ilmradi huu urasimu wa kusomesha watu halafu hamuwapi ajira hata za kujitolea tu ilimradi Wapate uzoefu inauma sana.


Mimi katika kifo nawazaga mno nitakufa nikiwa na umri gani 30-40?,50-60? Hilo ndo waga swali kuu na je kifo Cha namna gani kitanipata he na Nini baada ya Mimi kufumba macho Nini kinafuata kwenye hii system niliyonayo Sasa hv nafsi na roho.na itakuwaje siku hiyo ikija ghafla hata kesho nitaweza kweli kupona katika hukumu ya MUNGU.

Mimi katika afya nawazaga Sana huenda Nina kansa tayari au maradhi mengine kwa sababu ya life style niliyopitia katika huu ujana sema hata Kama nikiwaza Sina la kufanya naachia asili ichukue nafasi take.
Mimi katika utajiri sometimes nawazaga niwe na hela nyingi Kama diamond akitembea na team yake na mabodygurd 15..lakini pesa hio ya utajiri nawazaga nije kuotea jiwe Kama laizer.Nataka pesa nyingi za fasta ila za kiuhalali.

Mimi katika mavazi nawazaga ipo siku nitakuja kununua likitambaa likubwa nishone mashati mengi Kama 10 hivi.ina maana me nitakuwa na sare yangu yaani Shati la rangi moja tu ndo inakuwa Kama fashion yangu Tena rangi yenyewe nishaiwaza Ni blue.

Mimi katika huruma nawazaga Sana maisha ya binadamu wenzangu sijui niseme watumwa zangu.. inshort nafanya biashara ya kuuza sigara na pombe.nauzia vijana wenzangu Wengi kila wakija napata uchungu sawa naingiza pesa lakini bado roho inanisuta wakifa nahisi Mimi nitakuwa miongoni mwa waliosababisha vifo vyao.

Mimi katika ukali nawazaga Sana ingelikuwa Mimi Ni rais nina uwezo wa kutoa Siri za Serikali Basi siku moja ningetoa hotuba nzito ya kitaifa nikaweka wazi kuelezea kilichotokea katika Serikali mpaka ikafikia hatua kukawa Kuna Richmond,heroine kwanini Kama Serikali Ni ya watu kwanini kisinuke tu Mambo yote yawe yanawekwa wazi kwa 100% yaani maovu yote yamulikwe yote mpaka la kiongozi kupigwa risasi,ukweli juu ya hali ya maisha na uchumi wa taifa, mchakato wa Katiba mpya,n.k

Mambo Ni mengi Sina uhakika Kama na yenyewe yananipa stress au ndo level yangu hii natakiwa niwaze madude Kama haya.
 
Ok boss tunashukuru kwa taarifa...

Ila jitahidi uwe unatengeneza hoja/hadithi zako kwa paragraph...au shule yenu hamjasoma Imla Boss!????

Unawapa sana mods kazi..au hutaki MB zako ziyeyuke? Wee ni Masawe eeeh???
 
Ok boss tunashukuru kwa taarifa...

Ila jitahidi uwe unatengeneza hoja/hadithi zako kwa paragraph...au shule yenu hamjasoma Imla Boss!????

Unawapa sana mods kazi..au hutaki MB zako ziyeyuke? Wee ni Masawe eeeh???
Jf is where we talk openly.hoja mbona zipo wazi we pambana tu na hali yako utailewa vzr hoja yangu
 
Jf is where we talk openly.hoja mbona zipo wazi we pambana tu na hali yako utailewa vzr hoja yangu
Sijajua kama umenielewa au kama utanielewa..Hoja yako ni nzuri.

Ninachozungumzia mimi ni mpangilio wako wa maneno unayakusanya kama mafungu ya mchicha.

Ndo maana nikakwambia kwa sabbu mimi na wengine huwa tunavutiwa na hoja nzuri kama hizi kutoka kwako ndege JOHN na wengine humu jitahidi bhasi kuachanisha nafasi Mzee Baba tupate mavitu kutoka kwenu.

Au hapa nimekutukana tena Mzee mwenzangu!?
 
Usiwaze kazi na sala.niko vizuri sema tu malomoni kibao yamejaa kichwani ila mdogomdogo tutafika mzee baba.next time nitakuwa makini zaidi
 
Kwani mkeo ushaachana nae mkuu.

Najua ulizama Sana chumvini ndo maana unahofia cancer.

We live to die Acha mawenge.
 
Kwani mkeo ushaachana nae mkuu.

Najua ulizama Sana chumvini ndo maana unahofia cancer.

We live to die Acha mawenge.
Hilo pia lipo Ni miongoni Ila nayohofia Zaidi Ni katika mfumo wa digestion pombe Kali,smoking.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…