Mambo ya Darasani

jangala

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
1,583
Reaction score
2,365
Darasani huwezi kosa watu wafuatao:
1. Mrembo wa darasa.
2. Playboy/playgirl. Hawezi kutembea na msichana/mvulana mmoja mara mbili.
3. Group ya marafiki watatu. Kila mara wako pamoja.
4. Mtu mwenye maswali ya kuudhi/kukera.
5. Msongolist kimeo. Huyu huwa anasoma sana bt hana bahati ya kufanya vizuri. Yani msuli tembo, bt matokeo sisimizi.
6. Mlafi. Huyu huwa hakatai offer.
7. Mtoro wa kudumu. Haji darasani hata km hana sababu.
8. Mchelewaji wa kudumu. Anakuja kipindi kiko katikati au kinakaribia kuisha.
9. Miss/Mr.Misifa. kila mara ataeleza the way nyumbani kwao walivyo matajiri.
10. Less talkative bt kiwembe. Jamaa mkimya bt unakuta ametembea na karibu wasichana 15 hapo class.
11. Handsome boy ambaye hana mpango na wanawake.
12.Chips addicted. Hawa wanaweza kula chips asubuhi mchana na jioni. Jumatatu hadi jumatatu.
13. Back benchers. Hawa huwa watundu sana na ni watu wa jokes. Huwa hawajibu swali, but wanasubiri wakati wa kushangilia waongeze bezi.
14. Wambea. Hawapitwi na kitu darasani na washazoea kufeli.
15. Mchungaji/Mtumishi wa Mungu,
16. Waimbaji/Wasanii,
17.Walevi
18.Mabishoo.
19. Team popo. Hawa wewe na hela wasiwe na hela wanakesha club,
20.Mwenye aibu kusimama mbele za watu. Wakati wa Presentation anakimbilia kusimama nyuma ya wenzie,
21. Viherehere. Hawa mara nyingi hutokea kupendwa sana na waalimu.
22. Wanaosoma ili kushindana kwny GPA.
23. Kupe. Huyu boom likitoka atawaganda wenzie hadi ziishe, halafu yeye anaanza kula zake alone.
24. Wise man/woman. Huyu huwa ni mtu anayeaminika na kila mtu darasani. Hutumika sn kushauri pale mambo yanapoenda mrama. Mara nyingi huwa ni mtu mzima.
25.mpenda supu" yeye hata ya nyani atakunywa tu.
26.Fix man. Huyu atakuomba jero, akafuatilie dili la milioni kumi town, kumbe hana hela ya chai.
27. Photocopy machine. Huyu ukimuonesha majibu kwny mtihani anaweza kucopy hadi jina lako.
Usposema wewe uko namba ngapi mwngine atakusema
 
28. Mwanafunzi mchawi au mtoto wa mchawi au mjukuu wa mchawi.
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji100] [emoji100]
 
ahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaa!!!!!!!!!!!!!!!!!! uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ngoja waje wajieleze wako kundi gani.me usiniulize japo nilikwepo
 
ahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaa!!!!!!!!!!!!!!!!!! uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ngoja waje wajieleze wako kundi gani.me usiniulize japo nilikwepo
Mtu aliyesoma lazima awemo humo....
 
29. ma'snitch , hawa mnacheka nao kumbe wana wa spy tu ili wapeleke taarifa ofisini.
30. misuli mirefu, hana mda na mishemishe nyingine ye mda wote ni kusoma tu.
31. silint killer, huyu hajulikani anasoma muda gani, muda wote ni bata au michezo na mabo ya ajabuajabu lakini likija pepa anatusua kama kawaida
 
Wewe kweli ulisomam shule...vipengele vinadhihirisha..
 
13 hapoo hata kama najua kujibu kwangu sumu had tcha anitaje jna pia ntasmama tu af nakaa sijajibu
 
28. much-know huyu anamjua kilamwanafinzi na historia ya kwao maranyingi waongo lkn wanakusanya kijiji
 
Wenye wivu na ufaulu wa wenzao, wasinzia darasani, waropokaji, wapenda kujitolea iwe kufanya usafi au adhabu huwa hawagomi, mademu wa mwalimu Fulani, wanao jiona wababe wa darasa kinguvu but kichwani hazimo
 
yani iyo no 7 & 8 Najiona mimi kabiiiisa yan daah...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…