Mambo ya kuepuka kufanya ukiwa pombeni

Mambo ya kuepuka kufanya ukiwa pombeni

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
1. Usiingilie wala kuamulia ugomvi wa watu hasa wa mwanaume na mwanamke.

2. Usiingilie na kucomment mazungumzo ya watu usiowajua.

3. Usiwe unatoatoa ofa hovyo. siku ukipigika utaona aibu kwenda bar.

4. Usiwe ukidharau wanywaji wenzako na kujiona wewe ni bora sana. waheshimu na kusalimia bila ubaguzi.

5. Usiwe unabisha na kujidai unajua kila kitu na kuzungumzia mafanikio yako kwa kukera. mara demu wangu hivi, mara gari langu vile, mara nyumba yangu nyokonyoko.

6. Usitake kujionyesha kwa kulazimisha kujulikana we ni nani. mwingine atataka watu wote wajue ye ni dokta, yupo benki. na wengine huvaa mitisheti ya kazini kwao.

Ongezea...
 
Usipende kunywa mpaka ukalewa bar ya mbali sana na nyumbani tena ukiwa peke yako
 
Usikubali pombe ikutawale, achana na siasa na mambo yanayomhusu Mungu.
 
Ukienda chooni maliza bia ukitoka chooni fungua Bia = equal to X✓
 
Back
Top Bottom