1. Usiingilie wala kuamulia ugomvi wa watu hasa wa mwanaume na mwanamke.
2. Usiingilie na kucomment mazungumzo ya watu usiowajua.
3. Usiwe unatoatoa ofa hovyo. siku ukipigika utaona aibu kwenda bar.
4. Usiwe ukidharau wanywaji wenzako na kujiona wewe ni bora sana. waheshimu na kusalimia bila ubaguzi.
5. Usiwe unabisha na kujidai unajua kila kitu na kuzungumzia mafanikio yako kwa kukera. mara demu wangu hivi, mara gari langu vile, mara nyumba yangu nyokonyoko.
6. Usitake kujionyesha kwa kulazimisha kujulikana we ni nani. mwingine atataka watu wote wajue ye ni dokta, yupo benki. na wengine huvaa mitisheti ya kazini kwao.
Ongezea...