Kamanda Kazi
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 2,613
- 795
Nitaeleza namna ambavyo watu wanene wanavyoweza kupunguza uzito na kuendelea kuwa na uzito unaoendana na urefu wa miili yao (Body Mass Index – BMI). Kabla sijaeleza mambo muhimu ya kufanya ili kuondokana kabisa (100%) na Tatizo la Fetma au Unene uliozidi napenda nitoe angalizo kwa wale wanaovutiwa na madawa au programu zinazotangazwa kibiashara kwamba zitawawezesha kupunguza uzito mkubwa katika kipindi kifupi. Hiyo ni HATARI kwa afya yako. Watalaamu wa Afya wanashauri kupungua uzito kilo 1 - 1.5 tu kwa wiki na sio zaidi ya hapo. Haya sasa tuangalie mambo muhimu ya kufanya ili kutokomeza kabisa tatizo la Fetma (Obesity) na Uzito mkubwa (Overweight):-
Juisi ya kutibu tatizo la candida (Candidiasis): Blendi kwa pamoja tango (gramu 50), ‘natural yourgut' (90ml), maziwa (90ml) na majani 8-12 ya minti (mint leaves). Weka chumvi kidogo kwa ajili ya radha na nyunyiza juisi ya limau, kisha kunywa. Yourgut husaidia kurejesha bacteria wa asili hivyo kutibu maambukizi ya candida. Vitamin na madini yaliyomo kwenye matango huimarisha kinga ya asili ya mwili iliyokuwa imeharibiwa. Majani ya minti yana mafuta (essential oils) yanayodhibiti fangasi au bacteria (antifungal properties). Juisi hii ni nzuri kwa wanawake ambao wamekuwa wakipatwa na tatizo la fangasi aina ya Candida.
Tembelea www.asiliyako.blogspot.com kwa masuala ya Afya na Tiba
- Mara tu unapoamka asubuhi kabla ya kula chakula chochote kunywa glasi moja ya maji vuguvugu. Unaweza kukamua ndimu moja na kumimina juisi ya ndimu kwenye hayo maji. Unywaji wa maji asubuhi kabla ya kula chakula chochote hufanya mwili kujiweka tayari kwa ajili ya kuanza ‘process' ya uyeyushaji chakula.
- Kula chakula cha kutosha asubuhi (big breakfast). Asilimia 80 ya watu wanene hula kiasi kidogo cha chakula. Hii ni kinyume chake kwa watu wembamba ambao asilimia 80 hula kiasi kikubwa cha chakula wakati wa kifungua kinywa. Hakikisha kifungua kinywa kiwe cha vyakula vya asili (organic foods) kama vile matunda: tufaha (apples), pears, nanasi, mabalungi (grapefruits), plums, peaches, prune, mkate, siagi mbichi (not pasteurized and not homogenized), maziwa, plain yogurt (no sugar or fruits in it), nyama , kuku, viazi (kiasi), kahawa, asali, nk.
- Kunywa maji glasi nane (8) kila siku. Maji huitajika mwilini kwa ajili ya kusafisha au kutoa uchafu mwilini.
- Fanya mazoezi ya kutembea kwa mguu angalau kwa muda wa saa moja kila siku.
- Usile chakula baada ya saa 12 jioni. Hii ina maana kwamba muda wako wa mwisho wa kula chakula cha jioni au usiku iwe saa 12 au kabla ya hapo. Usilale mpaka upitishe angalau masaa mawili tangu ule chakula cha usiku. Hii itasaidia kuupa mwili muda wa kuyeyusha chakula.
- Shughulikia tatizo la ongezeko au kuoteana kwa candida mwilini mwako. Kumbuka watu wanene hukumbwa na tatizo la kuoteana kwa wingi kwa fangasi aina ya candida. Kuoteana kwa candida hupelekea maambukizi mdomoni, kooni, kwenye njia ya mfumo wa chakula (digestive tract) na kwenye njia ya uke (kwa wanawake). Hivyo kupunguza uzito bila kwanza kuwashughulikia candida ni ndoto maana hata kama ukifanikiwa kupungua unene upo uwezekano mkubwa wa kurudiwa na unene.