Mambo ya kufanya ukiwa ugenini

Mambo ya kufanya ukiwa ugenini

Fohadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
772
Reaction score
2,421
Huu ni uzi maalum kwajili ya kukumbushana baadhi ya vitu vidogo vidogo ambavyo huwa tunavipuuza lakini kuna muda vinaweza kutucost sana na kutusababishia matatizo. Inaweza ikawa iliwahi kukutokea wewe au jirani yako.

Binafsi naanza kwa kuwapa mbinu mbili:-

1. Ukiwa ugenini au sehemu yoyote ambayo hujulikani, let say labda umehamia huo mtaa siku za karibuni au umekuja kumtembelea ndugu, jamaa au rafiki. Tafadhali, usipende kupita njia za vichochoroni maana yake unaweza jikuta umetokea kwenye kibaraza cha mtu na yakakukuta. Jitahidi tu kupita main road. Waswahili wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha.

2. Ugenini au sehemu yoyote ambayo hutambuliki au hujulikani kwa wakazi wa hilo eneo, ogopa sana kutembea usiku mwingi peke yako bila mwenyeji.​

Chukua hii..usiseme sikukwambia.

 
Haya mkuu maana mi mwenyewe nipo mkoa wa mwanza kikazi na nina wiki tu...
 
Back
Top Bottom