Mambo ya kujiiba yanaumbua jamani afadhali uwe mkweli

Lokissa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Posts
7,445
Reaction score
2,500

Mke wa Frank anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi
videmu. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za
dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani
asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Frank
akabisha lakini taxi ikafika. Gonga Club & Lodge.

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, "Mambo Frank!" "Poa"

"Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu?" mke akauliza

"Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time
hapa" akajibu Frank

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager.
Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza,
"amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?"

Wakati Frank anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba
akawa amefika na kuuliza.

"Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji
nitawaletea huko huko"

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama
chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.
Wakati anapatana bei na dereva, Frank naye akaingia. Mama
yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga
kwikwi akamsikia dereve anasema.

"Duh, eee bwana Frank huyu mwanamke uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa!"

mamaa akazimiaaaazzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

hiyo ndio faida ya kumsifia mumeo bila kumchunguza.
 
Mara ya tatu hii inakuja hapa.

Asante kwa kunikumbusha
 
Mhhh ok mm sijawahi iona basi ipoteezeeni na msikasirike lengo ni kuwapasha habari kila zinapopatikana.hata bbc au cnn wanarudia habari zao kuanzia asubuhi hadi kunakucha 24 hrs a day.
 
Mhhh ok mm sijawahi iona basi ipoteezeeni na msikasirike lengo ni kuwapasha habari kila zinapopatikana.hata bbc au cnn wanarudia habari zao kuanzia asubuhi hadi kunakucha 24 hrs a day.

Mie nimekushukuru kwa kunikumbusha.

Usijali bana sawa?
 
Mie nimeiona kwa mara ya kwanza. Imetulia kweli kweli
 
Kuongea ni DHAHABU ila wakati mwingine kukaa kimya ni ALMASI. Hii kitu kila siku tunaijadili kinachofanyika ni kubadilisha heading.
 
Saafi sana, hawa wanaoonekana wapole na wataratibu ni wa kuwaangalia mara 2 sio njemba tu hata wadada.
 
Mabaya sana ulikuwa hujui??? hayafaikabisa
 
Mhhh ok mm sijawahi iona basi ipoteezeeni na msikasirike lengo ni kuwapasha habari kila zinapopatikana.hata bbc au cnn wanarudia habari zao kuanzia asubuhi hadi kunakucha 24 hrs a day.
Mi nashinda sana majukwaani hapa, lakini ni kwa mara ya kwanza naiona hii.
Imenifurahisha kishenzi, na inanikumbusha mambo fulani ya ujana!
 
Wasanii sio wote wako kwenye movie za kina Kanumba!
 
Halafu watu kama hawa wanaojifanya watakatifu huwa wanaumbuka vibaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…