Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 208
- 91
Kama nchi, ili tuendelee tunahitaji kufanya maboresho ya mara kwa mara ya sera za nchi ili kuendana na mabadiliko makubwa yanayotokea kila mara kadri wakati unavyoenda.
Kuna sera zilionekana kuwa bora wakati tunapata uhuru na miaka kadhaa baada ya uhuru, lakini kutokana na wakati, mabadiliko ya mifumo, sayansi na teknolojia, mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu na ongezeko kubwa la watu, sera hizo sasa zinaonekana kupitwa na wakati au kutokukidhi mahitaji ya sasa na kutokuendana na wakati uliopo.
Baadhi ya sera au masuala yanayohitaji kufanyiwa maboresho au marekebisho ili kuendana na wakati uliopo sasa, na Kuchochea maendeleo ya taifa na ya mtu mmoja mmoja ni kama ilivyoelezwa hapo chini.
Ukomo wa mihula ya kugombea ubunge iwe ni mihula minne ikiwa Mbunge atashinda mihula hiyo mfululizo au kwa awamu awamu, ili kutoa nafasi kwa watu wengine hasa kwa kizazi kipya chenye maono tofauti na namna tofauti ya uongozi na uwakilishi kuweza kuleta mabadiliko katika namna ya uongozi na uwakilishi na kutumia uwezo na maarifa tofauti waliyo nayo.
Kubadilishwa kwa adhabu ya Mbunge kufungiwa kushiriki vikao vya Bunge anapotenda kosa huko bungeni.
Mara kadhaa baadhi ya wabunge wamekuwa wakifungiwa kushiriki vikao vya Bunge pindi wanapokutwa na tuhuma za kukiuka taratibu na maadili ya bunge.
Hii ni kuwanyima wananchi haki yao ya kuwa na muwakilishi bungeni, na adhabu hii inamaanisha Bunge limewaadhibu wananchi wa jimbo husika na sio Mbunge aliyetenda kosa, kwa sababu Mbunge anapokosa kuhudhuria vikao maana yake shida na kero za wananchi wa Jimbo lake zinakosa msemaji, wananchi wanapokosa muwakilishi bungeni ambaye ndio msemaji wa kero na changamoto zao ni kuwanyima haki yao ya kikatiba na kutowatendea haki. Hivyo itafutwe adhabu nyingine tofauti na hiyo, adhabu hiyo inawaumiza na kuwakandamiza wananchi moja kwa moja.
Wagombea wa nafasi ya urais watumie dira ya taifa na sio ilani ya vyama vya siasa. Kwa sasa wagombea wa nafasi ya urais hunadi ilani za vyama vyao wakati wa kampeni za kugombea urais, wagombea huelezea ilani za vyama vyao na kueleza namna watakavyotekeleza Yale yaliyomo kwenye ilani mara baada ya kuchaguliwa na kushindwa urais.
Kwa wakati tuliopo sasa sio tena wa kutumia ilani ya chama ambayo ni maoni ya watu wachache kadri ya matakwa yao, iandaliwe dira ya taifa (kwa kukusanya na kuchambua maoni ya wananchi na kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo kwa wakati husika) kila baada ya miaka mitano ya uchafuzi mkuu inayoelekeza mambo muhimu ya kutekeleza na namna ya utekelezaji wake ndani ya miaka mitano, ili kama taifa tuwe na muelekeo wa pamoja na sio maono ya chama kimoja cha siasa kitakacho shinda kiti cha urais.
Kutumia ilani ya vyama vya siasa inaleta changamoto sana hasa katika kuharakisha maendeleo kwa wanachi, kwa sababu vyama vya siasa vinalenga kwanza kushika dola na kuendelea kubaki madarakani, lakini kama kutakuwa na dira ya taifa, mgombea yeyote atakayeshinda bila kujali chama alichotokea itambidi atekeleze mpango wa dira ya taifa ya miaka mitano na sio ilani ya chama chake. Hii itasaidia pia hata wakati ambapo chama pinzani kimeshinda nafasi ya urais bado muelekeo wa taifa utabaki palepale pasipo kuadhiriwa na mabadiliko ya uongozi na chama husika.
Waziri Mkuu asiwe Mbunge mwenye jimbo bali awe wa Mbunge wa kuteuliwa. Kwanza kabisa itampunguzia majukumu ya kijimbo na kumfanya kuwa na mda wa kutosha wa kutimiza majukumu ya kitaifa kama Waziri Mkuu na kupunguza mgongano wa kimaslahi wakati wa kutekeleza majukumu yake, tofauti na akiwa Mbunge mwenye jimbo.
Sherehe za uhuru, muungano na mbio za mwenge zifanyike kila baada ya miaka mitano. Kwanza, Itasaidia kupunguza gharama za kufanya sherehe na kukimbiza mbio za mwenge kila mwaka na fedha hizo kuelekezwa katika miradi mingine ya maendeleo, pia itatoa nafasi ya kufanyika kwa tathmini ya kina ya wapi tulipotoka, tulipo na kunapoelekea ndani ya hiyo miaka mitano, ili sasa wakati wa sherehe hizo kama taifa tujitathmini kwa kipindi cha miaka mitano tumepiga hatua gani na sio kila mwaka, pia wakati wa sherehe hizo yaonyeshwa mafanikio yaliyofikiwa kwa kipindi hicho chote na changamoto zilizojitokeza wakati wa kufika/kutekeleza mafanikio hayo ni siyo kama ilivyo sasa, tunaona kila wakati ni watoto wa halaiki, wasaini wa muziki na gwaride za kijeshi, sidhani kama hili ndio lengo la maadhimisho ya sherehe kama hizo.
Watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 au waliostaafu wasiteuliwe tena kwenye nafasi yoyote ile, ili kulinda nafasi za ajira kwa wengine na kuruhusu kizazi kingine kuonesha na kutumia uwezo walio nao. Imekuwa ni kawaida mtu anapostaafu nafasi fulani baadae tena unasikia ameteuliwa kuhudumu katika nafasi nyingine, huu ni ubinafsi mkubwa, ulafi wa madaraka na kushindwa kutambua kuwa kuna watu wengine pia wenye uwezo na sifa za kushika nafasi hizo na wakafanya mambo makubwa, mazuri na mapya zaidi ya watu walewale kuwa wanazunguka kwenye nafasi za uongozi huku kukiwa hakuna mabadiliko yoyote chanya wanayoleta kwa taifa. Mtu akistaafu nafasi aliyokuwa nayo, aachwe akapumzike ili watu wengine pia waendeleze gurudumu.

Upvote
10