Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Matukio ya kutisha na ya kishetani, kama yale ya utekaji wa watu na kuwapoteza, watoto wadogo kuuawa, kutawaliwa na watu wenye mioyo ya ukatili wa kupindukia, uovu kupewa heshima dhidi ya wema, ni ishara kuwa, yamkini nchi yetu ipo katika laana kwa sababu imetiwa unajisi na damu za wasio na hatia. Jambo la kujiuliza, tumefikaje hapa? Laana hii imetokana na nini?
Kwa wanaoamini uwepo wa Mungu wetu, muweza wa yote na mkuu wa kila kitu, wanaweza kurejea katika mafundisho ya kiimani na Biblia Takatifu kuhusiana na uovu wa umwagaji wa damu za wasio na hatia.
Hesabu 35:33: "Msiinajisi nchi mnayoishi. Umwagaji damu hunajisi nchi, na upatanisho hauwezekani kufanyika katika nchi ambayo damu imemwagwa, isipokuwa tu kwa damu ya yule aliyeimwaga damu"
Nchi hii kuna watu wengi wamepotea na kuuawa tena bila hatia. Tunaambiwa damu za wasio na hatia zikimwagwa zinaitia nchi nzima unajisi.
Mkumbuke matukio ya watu kutekwa na kuuawa hapo awali yalikuwa machache sana, lakini sasa yameongezeka maradufu kiasi cha baadhi ya watu, hasa wenye mamlaka, kututaka tuyaone kuwa ni matukio ya kawaida. Yaani tusione ajabu mtu kutekwa na kupotezwa au hata kutekwa na kuuawa na kisha mwili wake kutupwa porini Katavi na kwingineko ukaliwe na wanyama.
Ndiyo maana watawala huwezi kuwasikia wakitoa sauti kuonesha kuhuzunishwa na matukio haya ya kishetani. Ukiona wanaongelewa basi mpaka wawe wameulizwa.
Pia soma: Kuua ni laana hata vitabu vya vidini vimesema hivyo, usikubali kubebeshwa dhambi hiyo