JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Viongozi wa Dini wana nafasi kubwa ya kuikinga jamii dhidi ya maambukizi ya #CoronaVirus
Wizara ya Afya imetoa muongozo ambao Viongozi wa Dini wanapaswa kuuzingatia ili kudhibiti maambukizi ya #CoronaVirus
1: Hakikisha unatoa elimu kwa waumini kuhusu #COVID19
2: Hakikisha kwenye nyumba ya Ibada kuna sehemu ya kunawia mikono
3: Waumini wanawe mikono kwa Sabuni na Maji tiririka kabla ya kuingia kwenye Ibada
4: Idadi ya vipindi vya ibada iongezwe ili kuepusha msongamano
5: Waumini wakae umbali wa hatua 3 kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
6: Hakikisha Waumini hawapeani mikono kabla, baada au wakati wa Ibada
Upvote
0