Uchaguzi 2020 Mambo ya kuzingatia ili usipate usumbufu siku ya kupiga kura

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124


Ibara ya 5 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa haki kila raia aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura.Kwa mujibu wa vifungu vya 13(1), 13 (2), 35C, 61 (3)(a) na 63(1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 pamoja na kifungu cha 38 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani), Sura ya 292,Ili mtu aweze kupiga kura anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

(i) Awe amejiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura:

(ii) Awe ana Kadi ya Mpiga Kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi;

(iii) Awe katika kituo alichojiandikisha kupiga kura

Sheria ya Taifa ya uchaguzi inamruhusu mtu kupiga kura kwa kufuata utaratibu ufautao:

(i) Mpiga Kura anatakiwa kwenda kwenye kituo cha kupigia kura alichojiandikisha akiwa na kadi yake ya kupigia kura.

(ii) Mpiga kura anatakiwa kupanga mstari akiwa kituo cha kupigia kura na kusubiri hadi zamu yake ya kupiga kura itakapowadia.

(iii) Mpiga kura anatakiwa afuate maelekezo yote atakayopewa na msimamizi wa kituo muda wote akiwa kituoni.

(iv) Baada ya kumaliza kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kurudi nyumbani.
 
Upvote 1
Nimejiandikishia Arusha niko Dar naruhusiwa kupiga kura ya urais tuu. ???
 
Hiyo no (iv) kwa mwaka huu hapana kabisa..
Kurejea nyumbani ni baada ya matokeo ya kituo ulichopigia kura kutangazwa.
Pata picha kila anaeenda kupiga kura abaki hapo kusubiri matokeo. Ni kichekesho..
Halafu matokeo yanatoka Magu oyeee unarudi nyumbani na gubu loh
 
Issue sio mimi mana siko hata Dodoma
Nimewawazia waliohamishiwa Dodoma na ndio serikali yenyewe
 
Baadae itabidi kwenye electronic elections haya mambo ya kupiga ulipojiandikisha mmh...
 
Mimi nilijiandikisha kwenye draft la wapiga kura 2015 nikiwa Moshi, ila 2019 kipindi cha ku-update draftari la wapiga kura sikujitokeza.

Je mm bado nina sifa za mpiga kura ?
Ingia mtandao wa Tume hakiki kitambulisho chako kama kipo active
 
Baadae itabidi kwenye electronic elections haya mambo ya kupiga ulipojiandikisha mmh...
Marekani wana hadi early voting.,
Washaanza kuchagua na kuna foleni kabisa mtu ukipata muda unaenda.,
Japo the actual election day/final day ni November 4th

Kwetu tungeweza ruhusu kura ya rais ipigwe popote
 
Mimi sitarudi nyumbani , nitabaki kituoni na panga langu ili kulinda kura za bwana Magufuli zisiibiwe na mabeberu.

Mabeberu hawakawii kuja na maboksi ya kura zilizopigwa, safari hii CCM hatutakubali tena kuibiwa, tumeishaibiwa sana. Inatosha.
Mkuuu nimecheka Sana....
 
Mimi nilijiandikisha kwenye draft la wapiga kura 2015 nikiwa Moshi, ila 2019 kipindi cha ku-update draftari la wapiga kura sikujitokeza.

Je mm bado nina sifa za mpiga kura ?

Unaweza kuangalia kwenye tovuti ya NEC kama una kadi kwa kutumia no, utaona taarifa zako. Tembelea www.nec.go.tz
 
Kura zote kwa Tundu Lissu mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha Chadema!!
 
Hiyo no (iv) kwa mwaka huu hapana kabisa..
Kurejea nyumbani ni baada ya matokeo ya kituo ulichopigia kura kutangazwa.
Acha tusubirie muvi ya bure.............isije ikawa kama mikwara ya maandamano ya Kimambi
 
"Baada ya kumaliza kupiga kura mpiga kura anatakiwa kurudi nyumbani"

Kaah!

Sasa kuna ulazima gani wa kupiga kura si ni kama tu tumeuza hizo kura?

Kwanini tusingoje upigaji kura uishe zihesabiwe na tupate matokeo kwenye kituo chetu nani kashinda na kwa kura ngapi mbona ni rahisi tu
 
Hapa umenijibu hadi mimi nilikuwa Sina uhakika wa kupiga kura kwa sababu sijajiandikisha mwaka huu na kadi minayo ya zamani

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…