Mambo ya kuzingatia katika kuanzisha kidogo

Mambo ya kuzingatia katika kuanzisha kidogo

Joined
Mar 10, 2018
Posts
23
Reaction score
13
Assalam alaykum viongozi. Hope mko vizuri na mnaendelea vizuri na shughuli za ujenzi wa taifa.

Hizi kelele za kuelekea uchumi wa viwanda, tumezielewa vizuri tu, sasa kinachonipa maswali ni hatua zipi napaswa ili kufikia huko kwenye kiwanda kidogo.

Nahitaji msaada wenu wakuu hasa nyie mliofanikiwa kumiliki viwanda, lakini pia wataalam hasa wa shughuli za biashara. Me ni mwanamke wa uswahilini na mjasiriamali . Nafanya biashara ndogo ndogo na pia nafundisha wanawake wenzangu kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile Ubuyu wa Zanzibar, Udi, sabuni , mishumaa ,bidhaa za unga wa muhogo na nyingine kadha wa kadha.

Sasa baada ya kuelewa somo la viwanda, nahitaji kuwafundisha wenzangu juu ya hilo na pia binafsi nataka kuwa na cha kwangu. Pls naombe mnieleweshe step by step kwa mfano nataka kunzisha kiwanda cha mishumaa naanzia wapi? au kiwanda cha kutengeneza ubuyu , ili niwe mfanyabiashara halali naanzia wapi mwenzenu?

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom