Mambo ya kuzingatia katika ukuzaji wa vifaranga vya kuku

Mambo ya kuzingatia katika ukuzaji wa vifaranga vya kuku

belionea

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
1,052
Reaction score
915
Haya ni baadhi ya mambo muhimu sana kufanya kuanzia siku ya kwanza ili vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa.

i) Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye joto kwa wastani unaohitajika.

ii) Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na isiyokuwa na vimelea.

iii) Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks) siku ya kwanza.

iv) Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa kideri.

v) Inapofika siku ya 14, hakikisha vifaranga wanapata chanjo dhidi ya ugonjwa wa gumboro.

vi) Rudia chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.

vii) Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro.

viii) Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wa kuku wako wanapata chanjo ya ndui.

Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku wako ni salama na bora zaidi. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na mazao bora, na hatimaye kupata faida.

EX3osN0XgAAykg9.jpg
 
belionea,
Mkuu naomba kukuuliza,

Je, wewe unafuga na ulishawahi kulea vifaranga? Maana ulivyoandika inanipa mashaka kidogo.
 
Back
Top Bottom