SoC03 Mambo ya kuzingatia kupata Utawala Bora na Uwajibikaji katika Sekta ya Michezo Tanzania

SoC03 Mambo ya kuzingatia kupata Utawala Bora na Uwajibikaji katika Sekta ya Michezo Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Black fighter

New Member
Joined
Sep 5, 2021
Posts
2
Reaction score
2
MICHEZO ni shughuli ya kiburudani iliyopangwa kwaajili ya malezi na afya ya mwili.kuna aina nyingi za michezo kama masumbwi, mpira wa miguu, mpira wa magongo, mpira wa wavu, mpira wa pete, mpira wa mikono, kuongelea.

UWAJIBIKAJI ni kitendo cha mtu mwenye wadhifa kuchukua dhamana ya kosa lilofanywa na mtu ama yeye mwenyewe au mtu mwingine aliye chini yake.

UTAWALA BORA
ni matumizi ya mamlaka ambayo yanakuwa ya uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu, usawa na kufata usawa wa sheria.

YAFUATAYO NI MAMBO YA KUZINGATIWA KUPATA UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI KATIKA SEKTA YA MICHEZO TANZANIA;
KUANZISHWA VYAMA VYA MICHEZO
; Vyama vya michezo ni mashirika ambayo yana husika masuala ya kimichezo. Huwepo wa Vyama vya michezo utasaidia kuendesha michezo, kutatua changamoto mbalimbali za kimichezo, pamoja na kusimamia sheria na kanuni za michezo

UTOLEWAJI WA ELIMU; Elimu ni ujuzi wa utambuzi na uwezo wa kuwa na maarifa juu ya jambo hilo, viongozi wa michezo wanapaswa kuelimishwa kuhusu michezo ili kusimamia vyema na kwa ufanisi mkubwa wenye kuleta tija katika sekta ya michezo mfano kuandaliwa semina, maadhimisho na makongomano mbalimbali ya kimchezo.

USIMAMIAJI WA HAKI NA SHERIA ZA KIMICHEZO; Haki Ni kile kitu ambacho mtu anastahili kupata au anastahili kufanya au kufanyiwa na Sheria ni muongozo wa kikanuni unaotumiwa kuendesha haki. Haki inaitajika itendeke katika michezo ili kuimarisha michezo na kupunguza lawama na ukosoaji kama vile kutopendelea upande mmoja au washindi kupewa haki yao stahiki mfano Medali au kombe shindaniwa bila kujali ni jina, wala hadhi yao.

UHURU KUCHAGUA VIONGOZI BORA WA MICHEZO; Uchaguzi wa viongozi Ni hali ya watu kufanya chaguo binafsi la mtu akayewaongoza bila kushinikizwa na mtu yoyote. Itasaidia wanamichezo kupata mtu sahihi ambaye atakayesimamia na kuongoza misingi ya utawala bora na kuwajibika katika michezo.
N:B Uchaguzi huu uwe ni wa haki na uhuru pia kiongozi asiwe wa kudumu awe kila baada ya muda fulani(mf.kila baada ya miaka mitano 5).

MSAADA KUTOKA SERIKALI; Ni mchango kutoka kwa serikali. Serikali inahitajika kusaidia sekta ya michezo ili kukuza michezo mfano kama kuwaboreshea viwanja vya michezo, vifaa vya michezo na miundombinu mingine pia kuwezesha utolewaji wa elimu kwa kujenga shule na vyuo vya michezo ili kuandaa wataalamu wengi kwenye taaluma ya michezo.

KUPINGA MILA NA DESTURI POTOVU; mila na desturi potovu ni imani hasi za baadhi ya watu kwenye jamii.mfano baadhi ya jamii huamini kuwa michezo ni uhuni wakati sivyo bali michezo inadumisha amani na upendo. Tupapinga mila na desturi potovu kwa kutoa elimu na ushauri nasaha kwa wenye imani haba na jamii nzima kwa ujumla

KUBORESHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA; Sayansi na teknolojia ni miundombinu bora ya kisasa.Uwepo wa sayansi na teknolojia utasaidia kurahisisha baadhi ya mambo kama usafirishaji, huduma za afya, Elimu, umeme na maji na watu kupata ujuzi na weledi mpana katika kushughulika na mambo mbalimbali ya kimichezo.

KUUNDWA KWA TIMU ZA VIJANA(JUNIOR TEAM); ni kitendo cha kuwapa uzoefu wa kimichezo kizazi cha watoto watakaokuja kuendeleza timu za wakubwa. Kuundwa kwa timu za vijana kutasaidia kuibua vipaji mbalimbali ambavyo ni adhina kubwa ya baadae katika sekta yetu ya michezo nchini Tanzania.

KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUTANGAZA MICHEZO; Vyombo vya Habari Ni vitu ambavyo vinahusika kutoa taarifa mbalimbali zilizojiri au zinazoendelea katika jamii mfano redio, simu, luninga na barua na magazeti. Kwa Kutumia vyombo vya Habari kutangaza michezo kutasaidia kutasambazaa kwa urahisi na haraka taarifa za kimichezo katika jamii.

HITIMISHO
Michezo husaidia kuimarisha mwili akili, kuimarisha upendo na mshikamoo lakini pia michezo ni pia athari kama kusababisha majeraha au hata kupelekea vifo ila michezo pia husaidia kutoa fursa mbalimbali kama ualimu, udaktari na fursa zingine ambazo zinatainua maisha ya watu ambavyo kiasi kimoja au kingine itapunguza hali ya umasikini katika taifa la Tanzania.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom