Mambo ya kuzingatia kupunguza magonjwa yasio ambukizwa

Mambo ya kuzingatia kupunguza magonjwa yasio ambukizwa

jafari mwijae

Senior Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
181
Reaction score
39
NJIA KUMI ZA KUZUIA MAGOJWA YASIYO AMBUKIZWA
Magonjwa yasiyambukizwa ni magonjwa yasiyo na vimelea vinavyoweza kusambazwa.Mfano ni magonjwa sugu ya njia ya hewa ,kisukari,kuoza meno,magonjwa sugu ya njia ya hewa ,kisukari ,kuoza meno nakadhalika.
Zifuatazo ni njia za kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa.

1. Kila milo uwe na makundi yote tano ya vyakula Makundi hayo ni:

(a) nafaka/mizizi/ndizi mbichi za kupika
(b) Matunda
(c) Mbogamboga
(d) Jamii ya mikunde Na asili ya wanyama
(e) Mafuta.

2. Kula vyakula halisiSukari ikizidi mwilini huharibu mishipa ya damu Na fahamu, macho, Figo Na kongosho. Vyakula halisi huhifadhiwa Na kumen'genywa polepole tumboni ili sukari iliyopo ipatikane taratibu hivyo unashauriwa ifuatavyo:

(a) Usiongeze sukari kwenye vyakula au vinywaji kwani sukari hiyo hupatikana mwilini haraka zaidi ya inavyotakiwa. Pia sukari huchangia uozaji WA meno. Jumla ya sukari yote (kwenye vinywaji, chakula au chai) isizidi vijiko vidogo vya chai vitano Kwa mtu mmoja Kwa siku.

(b) Usikamue Matunda ili kuitengeneza juisi: tofauti Na juisi, Matunda hukaa tumboni muda mrefu zaidi Na kupunguza Kasi ya upatikanaji wa sukari mwilini.

(c) Usikoboe nafaka: magamba kwenye nafaka, Matunda Na Mbogamboga huzuia sukari isitiririke haraka tumboni.Kukoboa hupoteza protini, vitamini Na madini yaliyo kwenye magamba.Magamba husaidia kupata choo kingi na kwa urahisi na hivyo kuepusha sumu kurudi mwilini na kusababisha saratani ya utumbo mkubwa ,magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.Tunza nafaka vizuri .Ukungu una sumukuvu ambayo husababisha saratani ya ini.

3. USITUMIE MAFUTA MENGI
Mafuta yananaa Na yanaweza kuziba mishipa ya damu .Epuka Mafuta ya wanyama kwani Yana lehemu nyingi Na Ni rahisi kuganda; pendelea Mafuta kutoka mimea.

4. USITUMIE CHUMVI NYINGIChumvu isizidi kijiko kimoja kidogo Cha chai Kwa mtu mmoja Kwa siku.Ikizidi husababisha msukumo wa juu wa damu.

5. KULA TU KIASI ILI USINENEPEUzito (kg) isizidi urefu (cm) toa 100: Kwa mfano urefu ukiwa 163cm ,uzito isizidi 63kg .(163-100).Unene huongeza uwezekano wa kupata kisukari ,magonjwa ya moyo na mishipa ya damu,baadhi ya saratani na uharibifuwa viungo vya miguu na uti wa mgongo.

6. JISHUGHULISHE KILA SIKU
Jihusishe na chochote kitakachokufanya utoke jasho angalau kwa nusu saa kila siku.Usiketi mfululizo kwa zaidi ya saa moja .Simama ,jinyoshe au tembea hata kwa dakika 2 tu.

Bila mazoezi ,misuli hupoteza uwezo wa kutumia sukari, husinyaa na mifupa huwa laini na kuvunjika kwa urahisi.Mazoezi pia hupunguza msongo wa mawazo na chumvi na Mafuta mwilini.

7. TAMBUA UWEZO WAKO
Kuwa na malengo sahihi juu ya maisha yako na fanya tu yaliyo kwenye uwezo wa vipaji vyako ili kupunguza au kutawala msongo wa mawazo na kuepuka kisukari ,msukumo wa juu wa damu ,baadhi ya saratani na mlipuko wa magonjwa ya akili.

8. JIPATIE USINGIZI WA KUTOSHA Sio chini ya saa Saba Kwa mtu mzima mfululizo kila siku Kwa mtu mzima .Wakati umelala mwili hupumzika, hujikarabati Na kujitaharisha Kwa siku inayofuata.

9. EPUKA TUMBAKU NA ULEVI
Moshi wa sigara, shisha na hata ugoro vyote hudhuru sehemu nyingi za mwili na ni sababu kubwa ya magonjwa ya mapafu, moyo, kisukari na saratani nyingi. Ulevi ni gharama ni chanzo cha mivuragano, huchangia maambukizi ya magonjwa ya zinaa na ukimwi. Pombe inawwza kuharibu ini, kongosho, moyo na ubongo. Ukishindwa kuacha, usizidishe kipimo kimoja kwa siku kwa mwanamke au vipimo viwili kwa mwanaume.

10. CHUNGUZA AFYA YAKO ANGALAU MARA MOJA KILA MWAKA
Magonjwa mengi hudumu muda mrefu bila dalili huku yakiharibu mwili.Uchunguzi wa afya, hata pasipo dalili zozote, huwezesha tiba kabla ya madhara makubwa. Vilevile ni vizuri kila mwaka kupima ukamilifu wako. Makala hii imewathilishwa Dt Jafari Mwijae (Microbiota).
 
Back
Top Bottom