safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Afisa mikopo anashughulika na kuwapa watu mikopo,hivyo na sisi tunaopokea mikopo hiyo tunayo haki ya kujiita AFISA MADENI.
madeni ni katika sababu ya maendeleo kwani moja ya sababu ni kuwa WANAOKUDAI HUKUOMBEA UTOBOE ILI UWALIPE MADENI YAO,na Mungu mara nyingi hujibu dua hizo.
usikope kwa fasheni,kopa kwa mipango na mikakati ya nini utafanyia mkopo huo.
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia kwa Afisa madeni ili aishi vizuri na wanaoamdai
1. kama unatarajia kupata pesa tarehe 5 basi muahidi kumlipa tarehe 10,ila ukipata tarehe 5 mlipe tu.
hiyo itakuongezea credit na kumbukumbu nzuri kwa anayekudai hata ukienda mara nyingine atakukopesha kwa historia yako ya myuma,shida haziishagi.
2. Ukipata pesa bora umlipe kwanza kisha umkope tena,kuliko kwenda kumkopa tena huku ukiwa na Deni la nyuma haujalipa.
Lengo ni kumuondoa hofu ya kudhulumiwa mkopeshaji wako kwani muda wote anakuwazia kama utamlipa au laa.
Utafiti wangu unaonesha kwamba kabla ya kukopa mdaiwa huwa na wasiwasi kama atakopeshwa.
baada ya kukopeshwa basi wasiwasi ule unahamia kwa mkopeshaji akihofia kama atalipwa.
3. hakikisha mara kwa mara unamsalimia kwa simu au kwa kumtembelea huyo anayekudai.
Hiyo itampa imani kuwa Deni lake lipo sehemu salama na ataamini kuwa hautomdhulumu kwani wanaodhulumu mara nyingi huwa wanakata mawasiliano na wanaowadai.
KAMWE USIKATE MAWASILIANO NAYE
4. hakikisha wewe mdaiwa ndio unamkumbusha yeye kuhusu deni na hata katika kulipa hakikisha haanzi yeye kudai.
muwahi Yeye kumlipa kama ambavyo ulimuwahi mwanzo ulipoenda kumkopa.
5. hakikisha unamuaga pale unaposafiri kwa siku kadhaa(hata kama utarudi muage),asijeona tu haupo alafu anasikia kwa watu kwamba umesafiri.
6. Wakati bado haujalipa deni muombe ushauri wa mambo mbalimbali hata kama unajua solution yake we msikilize tu.
punguza ujuaji wa kila kitu mbele ya mwanaume anaekudai
7. hata kama yeye hajakuona basi anza wewe kumshtua na mpe salamu alafu endelea na mambo mengine.
kuna wakati anaweza kujifanya hajakuona alafu yeye akajua fika umemuona,so ukimpotezea atapata red flag kwamba unakimbia deni
8. Usimblock ama kumzimia simu peke yake,kama umeamua haupatikani basi usipatikane kwa watu wote hata akupigie nani.
sio unamblock yeye alafu akikupigia kwa namba nyingine anakupata,hapo unafeli.
9. Ukipata pesa tu mlipe chapu,ni bora uwe huna hela na hauna madeni,kuliko kuwa na hela na una madeni,haupati amani
10. Ukiwa unamlipa pesa zake usilalamike saaaana kuhusu shida zako,kwani hata yeye ana shida zake.
kulalamika kwako kutamfanya aone kwamba hsujspenda kulipa deni,so itakuwa ngumu pia kukukopesha kwa mara nyingine.
11. Usihofie kumlipa pesa Nusu hata kama tarehe tajwa haijafika(ikiwa hamkuwekeana sharti la kurudisha pesa yote kwa pamoja).
unaweza ukasema unasubiri upate yote alafu likatokea lingine la tarehe tajwa inafika hauna hata shilingi.so lipa hata nusu.
12. Kama haujapata pesa na tarehe imefika hakikisha unaandaa sababu ya kueleweka hata kama ni ya Uongo.
Sio unaenda kumuambia kwamba bhana pesa yako nilipata ila nilinywea pombe,atakuona mpumbavu.
Sababu za kijinga baki nazo mwenyewe ila kule andaa sababu za maana kwani inatosha sana wewe mweyewe ukijijua ujinga wako.
MWISHO : usijisifu sana kuwa una madeni,jisifu saaana kuyalipa madeni hayo.
ukomavu sio kuishi tu kwenye changamoto bali ukomavuvu ni kuishi ukizitatua changamoto hizo.
By safuher.