Mambo ya kuzingatia kwa wahitimu wa vyuo na watafuta ajira

Mambo ya kuzingatia kwa wahitimu wa vyuo na watafuta ajira

MwakiIV

Member
Joined
Aug 31, 2018
Posts
79
Reaction score
138
Umesoma mpaka level ya Diploma ama Degree.

Je, kuna ujuzi/ maarifa gani umejifunza kibinafsi ili ikuwezeshe kupata ajira au biashara yako mpya kesho? Soko la ajira au ulimwengu wa biashara unataka ujuzi au maarifa ya ziada, husiwe na kitu ambacho kila mmoja anacho.

Mara nyingi vitu vya aina hii vinakupa nafasi ndogo ya kuonekana bora. Hivyo tumia muda mwingi kujielimisha jambo au kufanyia utafiti kitu unaona kitaongeza tija kwenye elimu uliyoipata chuoni.

Dunia ina makapi mengi husikubali kuwa sehemu ya makapi, una nafasi kila siku kujiongezea ujuzi na maarifa ya jambo au kitu fulani

Kila la kheri ulimwenguni.
 
Back
Top Bottom