Mambo ya kuzingatia kwa Walimu wapya wakati wa kuripoti kazini

Fredrick Mmari

Senior Member
Joined
Jul 8, 2013
Posts
144
Reaction score
37
TAARIFA KWA WALIMU WAPYA KABLA YA KURIPOTI KWENYE VITUO VYAO VIPYA VYA KAZI.

Ndugu wadau wa taaluma hii ya ualimu kwanza nipende kutoa pongezi kwa wale wote ambao wameweza kupangiwa vituo vyao vipya vya kazi,haijalishi umepangiwa wapi na serikali ila kikubwa ni kupata nafasi ya kazi kwanza na mengine ndio yatafata baadae.

Pia napenda kutoa pole kwa wale wote ambao mpaka sasa hawajayaona majina yao ila bado wanayasubiri.Naomba mzidi kuwa na subira juu ya hilo ingawa inaumiza sana.

Leo nimeona ni vyema kuwapa taarifa muhimu wale wote ambao wamepata nafasi katika vituo vyao vipya vya kazi ya kufundisha.

Haya ni mambo muhimu yakuzingatia kabla hujaripoti kwenye kituo chako kipya cha kazi:

1.Mpaka sasa halmashauri nyingi zimeshatoa majina ya shule unayotakiwa kufundisha.Kwahiyo kwa wale wote ambao majina yao yalitolewa bila kuonesha umepangiwa shule gani,unaweza kuwasiliana na mtu yeyote aliye kwenye halimashauri husika akuchekie jina lako kwenye mbao za matangazo za hiyo halmashauri ili ujue umepangiwa shule gani.
Kama halimashauri yako hawajayaweka basi ni maswala yao tu ya utendaji huenda hayajakaa vizuri.



2.Kuna vitu vya kubeba ambavyo vinatakiwa kuwasilishwa kwenye shule husika,navyo ni kama vifuatavyo:

Cheti chako cha kuzaliwa.
Cheti chako cha kidato cha nne.
Cheti chako cha kidato cha sita kama utakuwa nacho maana kuna wengine waliunga diploma baada ya kumaliza certificate.
Cheti chako cha chuo pamoja na transcript.


3.Pia unaweza kubeba picha za passport size za ndugu zako au watu wako wa karibu unaotaka watengenezewe vitambulisho vya bima ya afya.Maana huwa kwa kawaida ni watu 6 ukiwa na wewe.Kubeba passport zao mapema itakusaidia kuokoa gharama za kuzituma tena wakati zinapohitajika maana natumai utakuwa mbali nao.


Mwisho niwatakie kila lakheri katika utendaji wenu mpya wa kazi.
 
Afu hivi hivyo vijihela vyetu vya kujikimu 2navichukulia wapi eti kwa mkuu wa wilaya ama? Hilo tu!! Loh !!
 
Hilo la bima ya afya mnatakiwa kuwa makini. Bima ya afya ni kwa mtumishi, mwenza wake na watoto wasiozidi wanne. Usije ukapeleka za ndg au jamaa ili kujaza hizo nafasi then ikawa tabu utakapokua na familia yako.
 

Thanx for information mkuu, ila kwa nn umetofautisha hapo kwenye red?
 
Sio lengo kiongozi nadhani ni setting tu so ni vyeti tu kama vya juu vinavyohitajika
 
cheti na transript tofauti.
Cheti huwa kinaonesha GPA yako na kozi tu ila transcript kinaonesha vyote pamoja na kozi zoote ulizosoma mpaka unamaliza na alama zake ulizopata kwa kila kozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…