Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kama ilivyokuwa desturi ya Watanzania wengi kwenda kusalimia ndugu na jamaa mikoani. Inawapasa kufahamu mambo gani ya kuzingatia zaidi katika safari zako za kwenda kusalimia.
1. Tengeneza bajeti ya safari ikijumuisha gharama za usafiri, chakula, zawadi, na matumizi mengine ya nyumbani.
2. Beba pesa taslimu ya kutosha, hasa ikiwa unatembelea maeneo ambayo huduma za kifedha hazipatikani kwa urahisi.
3. Tafakari juu ya zawadi ndogo kama ishara ya upendo na shukrani, kama vile vyakula, vinywaji, au vitu vya matumizi ya nyumbani.
4. Hakikisha zawadi zinaendana na mahitaji ya wale unaowatembelea. Maana kuna watu wanabeba zawadi ambazo walengwa kwao zinakuwa azina faida yoyote kwao!
5. Usisahau kubeba dawa za msingi, hasa kama unatembelea maeneo yenye mazingira ambayo yanaweza kuwa na changamoto ya kupata huduma za kiafya.
6. Valia mavazi yanayostahili kulingana na mazingira ya kijamii ya wenyeji
7. Pangilia muda wa kurudi mapema ili kuepuka msongamano wa magari au ucheleweshaji wa usafiri. Maana hapa kuna watu inafika muda wa kurudi hata nauli unakuta awana au tiketi awajakata inafika hatua wanajutia safari yenyewe.
8. Weka muda wa kutosha kusikiliza changamoto au habari kutoka kwa ndugu zako.
9. Hakikisha unazingatia usalama barabarani kama unaendesha gari au upo kwenye basi la abira inakupaswa kukumbusha utulivu mkubwa. Ili kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza kwa uzembe!
Yangu ni hayo kwa leo kama na wewe unayako basi ongezea hapo! Kulingana na tamaduni za kwenu pia itapendeza zaidi.
Kumbuka: Nyakati za sikukuu ni fursa nzuri ya kuimarisha mahusiano ya kifamilia. Ukizingatia mambo haya, utaifanya ziara yako iwe yenye maana na furaha kwa wote.