Mambo ya kuzingatia unapochagua mavazi kwa ajili ya sherehe

Mambo ya kuzingatia unapochagua mavazi kwa ajili ya sherehe

Queen V

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
775
Reaction score
1,332
1. Zingatia aina ya sherehe na rangi

Je, ni sherehe rasmi, ya kuvaa kawaida au ya mavazi maalum(costume party)? Pia chunguza kama kuna rangi mahususi kwa ajili ya waalikwa na jitahidi kuijumuisha kwenye mavazi yako.

2. Zingatia eneo

Mavazi na viatu utakavyovaa kwenye sherehe ya ufukweni ni tofauti na vya sherehe ya hotelini

3. Hali ya hewa

Hali ya hewa ya siku na mazingira husika inachangia kwa kiasi kikubwa chaguo lako la mavazi. Upepo unaweza kuwa mkali na kukukosesha amani hasa mida ya usiku. Kama unaenda ugenini ni vyema kuuliza wenyeji kuhusu hali ya hewa kulingana na muda wa sherehe.

4. Usivae nyeupe kama si rangi ya sherehe

Kuna sheria inayodai watu wasivae nguo nyeupe kwa sababu ni mahususi kwa bibi harusi lakini kutovaa nyeupe si kwa harusi tu.

Nguo nyeupe huweka madoa inapomwagikiwa na vyakula na vinywaji na huweza kupelekea ukosefu wa amani.

5. Kuwa makini na nguo za ndani

Sherehe aghalabu huwa na wapiga picha kwa ajili ya matukio mbalimbali. Si vema nguo za ndani kama brazia zikaonekana kwa nje na hata kukuharibia picha zako


6. Vaa viatu vinavyokupa uhuru

Vaa viatu vitakavyokupa uhuru wa kuzunguka ukumbini na kucheza muziki bila kulazimika kuvivua au kubadili katikati ya sherehe
 
Back
Top Bottom