Mambo ya kuzingatia unapoendesha gari Mjini.

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2020
Posts
1,634
Reaction score
3,833
Habari jf
Naomba msaada Ni Mambo gani ya kuzingatia unapoanza kuendesha gari Mjini posta kariakoo na maeneo mbalimbali Mjini Kama dereva wa bolt na Uber ..

Karibuni Sana.
 
1. Angalia sana vibao vya "No Way" na "No U-Turn" etc

2. Heshimu sana sana Zebra na Mataa. Matrafiki wanajificha sana kwenye ayo maeneo.

3. Angalia sana unapopark. Utachubuliwa na wasukuma mikokoteni na magari ya mizigo.

4. Uwe full na Leseni, Kopi ya Kadi, Fire Extinguisher, Triangle Mbili.

5. Usiwe na madeni, lipia bima.

6. Usiwe bahili wa kutoa elfu 5 kwa trafic.

Hafu mbona Uber na Bolt hazipo mzee. We unaongelea Moovin au?
 
lock milango muda wote ikiwezekana funga vioo.
funga mkanda unapoendesha gari wewe na abiria au watu uliowabeba.
kuwa makini kuna matapeli wanavaa kiraia wanajifanya ni askari kisha wanakuzingua.
 
Bajaj Boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…