Mambo ya kuzingatia unaponunua tairi za gari

Kuna mambo kadhaa ya kuangalia baadhi ni
1. Size ya matairi. Matairi madogo husababisha injini kuzunguka zaidi.
2. Uendeshaji. Ukikanyaga sana xrator hupelekea rpm kuwa juu na ulaji mkubwa wa mafuta.
3. Air cleaner iliyochakaa
4. Umri wa gari nk
SASA KWENYE HIYO PCHA UNAZUNGUMZIA UPANA WA TAIRI AU UREFU WA TAIRI , maana kwenye picha zako tofauti ipo kwenye upana wa tairi na wala sio urefu.
Explanation pleaseee
 
upana unamaanisha nii mkuu, is it Rim Size au upana wa Tairi
 
Hapo umegusia tairi ndogo under the same rim size, je ukiweka tairi kubwa under the same rim size vp na lenyewe itakuwa inakula mafuta au inaserve
 
Msinione kimya mie nameza tu hapa leo. na hii inanihusu zaidi
 

Mkuu kwangu iliwaka hii alarm nikiwa kwenye motion na gari ikakataa kabisa comand zangu yaani no brake sterling ngumu na lilizima kabisa ilibidi kusali hadi nikafika kwenye muinuko kidogo ni nini hii mtaalam?
 
Ombi kwa MoDs.
Topic hii ibaki hapa kwa faida ya wana JF
Ingekuwa vizuri angeweka na ile inayoonesha tairi limetengenezwa lini na lina expire lini au baada ya muda gani. Maana nasikia tairi linakuwa na uhai wa mika 4 toka linapotengenezwa. Hivyo mtu anaweza kununua tairi jipya kumbe toka limetoka kiwandani lina miaka 4 au zaidi halafu akashangaa akifunga kwenye gari baada ya muda mfupi linapasuka. Wengi hawana utaalamu wakusoma maandishi na maana zake katika matairi.
 
wadau naombeni mnijuze na mimi matumizi sahihi ya overdrive ikiwa on au off
Hii hapa mtumishi tulia na uisome kwa makini itakusaidia.

FAHAMU MATUMIZI YA OVERDRIVE KATIKA MAGARI YA AUTO

OVERDRIVE NI NINI?
Overdrive ni gia katika mfumo wa gari ambayo uifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Overdrive ni kama gia ya ziada itakayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya engine yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea na mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo mana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya engine. Mfano katka gari ya kawaida yani 180km/h ili ufikishe speed 120km/h basi rpm inaweza kua 4000rpm. Katka barabara tambarare. ila ukiweka over drive unaweza tembea speed hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara tambarare.

UTAJUAJE KUWA OVERDRIVE IPO ON AU OFF?
Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako inamaanisha kuwa Overdrive ipo off na pindi Kitaa cha overdrive kisipoonekana basi overdrive ipo on.Overdrive imewekwa Kama option yakutumia wakati ukiwa unatembelea speed chini ya 60km/h.

MATUMIZI YA OVERDRIVE NI YAPI?
Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe gari yako inakuwa imepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukisha maliza tena matumizi yake.
Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au On na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gear kubwa na speed less than 60km kwahio unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.
 
Mwenye kujua title yake tafadhali anipatie nijifunzi zaidi
 
Mkuu, tairi zinaishi miaka 4 toka siku zimetoka kuivishwa kiwandani, so wanachoandika kwenye tairi Ni siku ilipotengenezwa, na wanaandika wiki ya ngapi na mwaka!

mfano (2414)- Hii maana yake ilitengenezwa wiki ya 24 mwaka 2014.

Au (1017) - Hii maana yake ilitengenezwa wiki ya 10 mwaka 2017,

So hapo sasa ukishajua imetengenezwa lini unahesabu miaka mi4 mbele ndo unakua mwisho WA maisha ya tairi husika.
 
UFAHAMU: KWA WENYE MAGARI;

Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari yako).

Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne.

Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. Kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999.

KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE.

Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi Kama ifuatavyo

CODE. SPIDI;
F========80
G ========90
J ========100
K ========110
L ========120
M ========130
N ========140
P ========150
Q ========160
R ========170
S ========180
T ========190
H ========200

Huandikwa hivi
280/R/70/13/560/S
Hapo herufi S inawakilisha spidi,180.
 
Mwenye kujua title yake tafadhali anipatie nijifunzi zaidi
Nataka kujua namna ya kujua expire date za matairi ya magari
- Angalia tairi imetengenezwa mwaka gani.
- Tairi iliyokaa kwa zaidi ya miaka 4 haifai kwa matumizi, hata kama ni mpya iko dukani.
- Kwa baadhi ya kampuni tairi zao ni hadi miaka 8

Je ni jinsi gani utatambua tairi ni lini imetengenezwa?
- Angalia hii Picha

- Ukiangalia namba za mwishoni hapo ni 2716 inatupa taarifa mbili
1. Mwaka ni 2016
2. Wiki ya 27 ya mwaka husika
Mwenye kujua tafadhali anitaarifu
 
i thought its was L for sloping to reduce your brake pads friction...
 
WE JAMAA NI KICHWA HATARI SANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…