JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTANGAZA BIASHARA MTANDAONI
Jifunze na uitambue hadhira yako unayoilenga
Ikiwa huijui hadhira yako ni ipi, huwezi kuipa kile inachotaka, na kisha nayo haitakupa kile unachotaka.
Wafahamu kwa umri wao, wanaishi wapi, wanazungumza lugha gani na wapo katika hatua gani ya maisha (mwanafunzi, mzazi, mstaafu)
Chagua ni mitandao ipi utumie na ipi ya kupuuza
Tafiti idadi ya watu wanaotumia mitandao hiyo. Hii itakusaidia kuamua ni mitandao gani utumie na ipi ya kuachana nayo.
Fahamu washindani wako; Kwa sababu ikiwa hutafanya hivyo, watapata nguvu. Pia, kujifunza kutoka kwenye kile wanachofanya, itakusaidia kuamua ni nini unapaswa na kipi hupaswi kufanya.
Jua ni kina nani, wako wapi, wanafanya nini, walifanya nini hapo awali, kama wanaleta vitisho vyovyote kwenye biashara yako, wako mitandao gani, hadhira yao ni kubwa na wanachapisha mara ngapi
Upvote
1