Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MAMBO YA KUZINGATIA UWAPO KWENYE MKESHA.
Anaandika, Robert Heriel.
Ikiwa Leo ni ukurasa wa mwisho katika kitabu cha mwaka 2021, siku ya leo sitakuwa na mengi ya kusema;
Mwisho wa mwaka ni mwanzo WA mwaka mwingine. Siku zinaenda nazo hazirudi tena, huja Kwa matumaini makubwa huondoka Kwa huzuni kuu. Huja na watu na mambo yake huondoka na wasiowake. Loooh! Basi tumche yeye aliyetuleta ingawaje hatumuoni.
Niite Taikon wa Fasihi, kijana niliyechanganyikiwa.
Kukesha tukiomba!
Kukesha tukilewa na kunywa pombe tukifurahi na kuburudika. Kukesha tukicheza muziki na kuimba nyimbo kuzifurahia siku zetu njema tungali tunayo Afya. Kwa maana Kama hatutafurahi Leo ni lini tutakayofurahi! Tazama siku ya Leo imekuja hivi nayo imetukuta tunazonguvu zetu, ndio maana tunafurahi na tuwapendao huku tukijihadhari na adui zetu. Hiyo kesho hakuna ajuaye. Basi tufurahi pamoja.
Watu hukesha Kwa mambo mawili. Hukesha Kwa furaha ambapo hufurahia mambo Mema na MAZURI. Husubiri siku njema, zawadi au Mgeni mwema. Lakini kupo kukesha Kwa Huzuni kumsubiri au kujihami na adui asijekukuta umelala akakudhuru na kukuangamiza.
Hata hivyo waweze Kesha Kwa furaha lakini adui akajitokeza Kwa ghafula. Nawe Kama hukujiandaa je hautapata madhara!
Kukesha kwenye mkesha! Mkesha wa waombaji! Mkesha wa walevi! mkesha wa Malaya na wazinzi! Mkesha wa wevi na wanyang'anyi. Mkesha
Hata hivyo ungali kijana Mdogo usiogope kukesha, kukesha kujifurahisha lakini pia usipende tuu kukesha kujifurahisha Bali upende zaidi kukesha kuzalisha Utajiri na akiba ya uzeeni.
Hata hivyo Usisahau walau mara Moja Kwa mwezi kukesha ukiomba na kumsifu Mungu aliyekuumba, tena ukiomba akupe kibali kila ufanyalo liende wala usikwame.
Kwa maana hakuna aliyewahi kufanikiwa Kwa lolote pasipo kukesha.
Haya niliwaambia sitasema mengi. Basi tunapoelekea kwenye Mkesha wa mwaka huu basi haya machache ni muhimu kuyazingatia;
Ikiwa kipato chako ni cha Kati kwenda chini kumaanisha Maeneo utakayoenda yatakuwa na ulinzi mdogo basi yakupasa uwe Makini zaidi ya Yule mwenye uchumi Mkubwa ambaye lazima atajitahidi aende kwenye mkesha mahali penye ulinzi na Usalama WA kutosha.
Jambo la Kwanza kwenye mkesha ni ulinzi na Usalama kabla ya mambo ya kufurahi na kuburudika.
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia uwapo kwenye Mkesha;
Uwapo kwenye mkesha, jitahidi ukae sehemu ambayo sauti yake ni yakawaida ambayo unaweza kusikia mzunguko mzuri wa sauti za wanaokuzunguka. Sio ukae karibu na maspika au mahali penye kelele nyingi.
Kaa karibu na dirisha ambalo unaweza kulitumia ku-escape. Au mlangoni ili iwe rahisi kwako kukimbia ikitokea dharura Kama ya uhalifu au Moto.
Hata Kama umeona Pisi Kali yenye matako na hipsi za haja. Jikaushe! Jizuie hivyo hivyo. Jikakamue kitaikon. Usishoboke na Mali mpya uwapo kwenye mkesha. Vinginevyo uwe umejipanga haswa uwe na backup ya kutosha. Hata hivyo kwenye mikesha na kumbi za burudani usipendelee kuanzisha Vagi Kwa kutegemea Backup ya Wana. Ipo siku inaweza kukugharimu.
VAA viatu simpo vinavyoshika miguu vizuri na ambavyo vinaweza kutumika kujihami na kupambana na ukizidiwa kukimbia. Nguo ziwe nyepesi.
Na hii zaidi ni Kwa wale wanangu wa matamasha ya Uswahilini tandale, Manzese, Temeke, mwananyamala, Kwa upande wa DSM. Mikoa mingine nanyi vivyo hivyo.
Katika matamasha ya mkesha au ya starehe usikubali kubananishwa na kuzongwa na watu usiowajua. Ni vizuri Kama mmeenda watano muzongane wenyewe Kwa wenyewe.
Yaani hata uone wanauana Acha wauane wewe usijiingize kwenye ishu usizozijua. Wengi waliojipendekeza imekula kwao. Waliishia kupata majeraha huku wengine wakipoteza maisha.
Kugombelezea waachie wenye kazi hiyo ambayo walioandaa Hilo tamasha wamewaandaa.
Usitoe toe mikono yako hovyo Kwa watu usiowajua. Kama utaona inakuzuia Sana basi mpe Mkono Kwa upande wa nyuma wa kiganja au mpe tano.
Kwenye mikesha kuna watu wanamichezo ya ajabu ajabu katika falme za rohoni.
Ila usijesema nimekuruhusu kuzini. Kuzini ni dhambi.
Sio unadandia dandia vyombo vya watu ambao hamkuwa na makubaliano yoyote. Sio vizuri.
Ukicheza Kwa kuangalia wengine utajiona hujui kucheza na hivyo utajikuta mara Kwa mara umesimama ukishangaa wenzako.
Kuwa Kama TAIKON akicheza haangalii upande wa pili. Niwe najua au sijui kucheza Hilo halinisumbui ili Mradi ninafurahia muziki.
Usipendelee kufanya zinaa na kuziacha Acha hovyo Manii zako ni hatari hasa kwenye matukio ya mikesha ya mwaka mpya.
Shahawa zako zina vinasaba vyako. Vinawewe. Kuviacha hovyo hovyo ni kujiachia hovyo hovyo. Ni kuuza usalama wako.
Naweza nisieleweke lakini ndivyo ilivyo.
Usikae kizembe zembe hasa uwapo Maeneo ambayo usalama ni mdogo hasa Kwa Sisi wenye vipato duni au vyakati.
Unaweza ukawahi kutoka kabla ya muda wa kutoka au ukachelewa ukawaacha watu watoke wote wenye haraka alafu msongamano ukiwa umepungua ndio utoke.
Hewa huwa nzito na magonjwa ya hewa ni rahisi kusambaa. Pia majasho ya watu mkigusana unaweza pata Maradhi ya ngozi. Ndio maana nalikuambia usiruhusu kusongwa au kubanwa banwa. Kwani sio salama kiafya na pia ni rahisi kuibiwa.
Taikon sina laziada. Nakutakia Mkesha mwema. Kheri ya mwaka mpya.
Nawashukuru Wale wote mliokuwa NAMI mwaka mzima. Mliosoma kazi zangu.
Kwa mahali nilipokosea mnisamehe kwani Mimi sina ziada kuliko wengine nami ni Binadamu Kama wengine. Ingawaje natokea nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo huku na Huku.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Palm Village, Mikocheni, Dar es salaam

1. Usikae sehemu yenye Sauti kubwa ya muziki au kelele nyingi.
Uwapo kwenye mkesha, jitahidi ukae sehemu ambayo sauti yake ni yakawaida ambayo unaweza kusikia mzunguko mzuri wa sauti za wanaokuzunguka. Sio ukae karibu na maspika au mahali penye kelele nyingi.
2. Kaa sehemu inayokuruhusu kuondoka Kwa upesi Kama itatokea dharura yoyote yenye hatari.
Kaa karibu na dirisha ambalo unaweza kulitumia ku-escape. Au mlangoni ili iwe rahisi kwako kukimbia ikitokea dharura Kama ya uhalifu au Moto.
3. Usishobokee wanawake/wanaume wa watu ambao huwajui/wasiokuhusu.
Hata Kama umeona Pisi Kali yenye matako na hipsi za haja. Jikaushe! Jizuie hivyo hivyo. Jikakamue kitaikon. Usishoboke na Mali mpya uwapo kwenye mkesha. Vinginevyo uwe umejipanga haswa uwe na backup ya kutosha. Hata hivyo kwenye mikesha na kumbi za burudani usipendelee kuanzisha Vagi Kwa kutegemea Backup ya Wana. Ipo siku inaweza kukugharimu.
4. Usivae viatu vizito na nguo zitakazokunyima Uhuru.
VAA viatu simpo vinavyoshika miguu vizuri na ambavyo vinaweza kutumika kujihami na kupambana na ukizidiwa kukimbia. Nguo ziwe nyepesi.
Kama ni kuenjoi enjoi. Usicheze chezee simu. Itakupotezea focus.5. Simu isikupotezee Tageti.
Na hii zaidi ni Kwa wale wanangu wa matamasha ya Uswahilini tandale, Manzese, Temeke, mwananyamala, Kwa upande wa DSM. Mikoa mingine nanyi vivyo hivyo.
6. Usibebe vitu vingi na wala usimuachie simu au kitu chochote mtu usiyemjua uliyekutana naye kwenye mkesha.
7. Usikubali kuzongwa na kuminywa minywa na watu usiowajua.
Katika matamasha ya mkesha au ya starehe usikubali kubananishwa na kuzongwa na watu usiowajua. Ni vizuri Kama mmeenda watano muzongane wenyewe Kwa wenyewe.
8. Usikubali kugombelezea au kukania ugomvi wowote usiokuhusu ukiwa Mkeshani.
Yaani hata uone wanauana Acha wauane wewe usijiingize kwenye ishu usizozijua. Wengi waliojipendekeza imekula kwao. Waliishia kupata majeraha huku wengine wakipoteza maisha.
Kugombelezea waachie wenye kazi hiyo ambayo walioandaa Hilo tamasha wamewaandaa.
9. Kama watu wamelewa Kwa kiwango kinachokaribia kupita kiasi. Usiache chupa ikatoka mkononi mwako. Cheza nayo, zunguka nayo, burudika nayo hata Kama chupa imeisha pombe.
10. Kama ni mkesha wa Dini. Usikubali mtu usiyemjua akuzoee Kwa upesi hasa kukushika Mkono wako.
Usitoe toe mikono yako hovyo Kwa watu usiowajua. Kama utaona inakuzuia Sana basi mpe Mkono Kwa upande wa nyuma wa kiganja au mpe tano.
Kwenye mikesha kuna watu wanamichezo ya ajabu ajabu katika falme za rohoni.
Asiwe msifie mhubiri au Kwaya au kusifia Huduma inayoendelea Kama sehemu ya kuomba urafiki wake kwako.11. Hakikisha aliyekaa jirani yako asiyaendeshe mahusiano yenu ya muda huo WA mkesha. Hasa mkesha wa Dini.
12. Kama utatongoza mwanamke au kutongozwa na Mwanaume hakikisha mnahusiana baada ya siku Saba kupita. Usiruhusu ukalala naye usiku huo huo. Au kesho yake au chini ya siku Saba.
Ila usijesema nimekuruhusu kuzini. Kuzini ni dhambi.
13. Hakikisha unajua usafiri utakaokurejesha salama nyumbani.
Sio unadandia dandia vyombo vya watu ambao hamkuwa na makubaliano yoyote. Sio vizuri.
14. Ukicheza usiangalie wengine wanachezaje. Wewe cheza tuu bila kujali.
Ukicheza Kwa kuangalia wengine utajiona hujui kucheza na hivyo utajikuta mara Kwa mara umesimama ukishangaa wenzako.
Kuwa Kama TAIKON akicheza haangalii upande wa pili. Niwe najua au sijui kucheza Hilo halinisumbui ili Mradi ninafurahia muziki.
15. Usinywe pombe mpaka akili ikakuvuka na usiache chupa ya via mezani Kwa watu usiowajua.
16. Kama utafanya zinaa. Hakikisha Shahawa zako ziwe sehemu salama.
Usipendelee kufanya zinaa na kuziacha Acha hovyo Manii zako ni hatari hasa kwenye matukio ya mikesha ya mwaka mpya.
Shahawa zako zina vinasaba vyako. Vinawewe. Kuviacha hovyo hovyo ni kujiachia hovyo hovyo. Ni kuuza usalama wako.
Naweza nisieleweke lakini ndivyo ilivyo.
17. Macho yako yasizembee kuziangalia nyendo za wanaokuzunguka.
Usikae kizembe zembe hasa uwapo Maeneo ambayo usalama ni mdogo hasa Kwa Sisi wenye vipato duni au vyakati.
18. Wakati WA kutoka usikubali kuwa kwenye ule msongamano.
Unaweza ukawahi kutoka kabla ya muda wa kutoka au ukachelewa ukawaacha watu watoke wote wenye haraka alafu msongamano ukiwa umepungua ndio utoke.
19. Kadiri watu walewavyo na wakaavyo watasweti. Usiruhusu kusongwa.