Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Namcheki Babu wa Loliondo kwenye taarifa ya habari TBC 1, na mmea huo wa utabibu wa magonjwa sugu unafanana na pareto.

Jamani sijui nijaribu kuchemsha maua ya pareto au sio wanajamvi?
 
Namcheki Babu wa Loliondo kwenye taarifa ya habari TBC 1, na mmea huo wa utabibu wa magonjwa sugu unafanana na pareto.

Jamani sijui nijaribu kuchemsha maua ya pareto au sio wanajamvi?

ule mti sio pareto bali mti mmoja ambao twiga wanapenda kule. Pareto ni sumu ucjaribu
 
maelezo gani? ina maana bosi kama anaumwa hawezi kwenda kujitibu? au auantaka magari yote ya serikali mpande wananchi wote hata kama haikuhusu
 
Huyu babu amenifanya nikumbuke maneno ya Mungu kuwa...' kiburi cha mwanadamu ni uzima', at the point of death kiburi chote cha mwanadamu kinayeyuka...Imagine watu wanaoinamiwa kwa heshima kede kede na wenye sauti za nguvu wote wamepewa amri ya kwenda kufoleni Loliondo na kibabu tu maskini bila kujali status ya yeyote (Aise Babu nakupongeza sana kwakutopenda ubaguzi) na wao bila hata kulazimishwa wakafuata amri ili tu wapate uzima. Sasa wahubiri tukisema kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kuwa Yesu ni bwana utashangaa mtu kwa kiburi cha uzima atakufanyia analysis mpaka unakaa chini...Ukiona mtu anachallenge decision ya wengine ujue ndani kuna kakiburi cha uzima kanasumbua ndiyo maana anaweza nyanyua kifua na kujidai yeye ana akili kuliko wenzake....Tumshukuruni Mungu kwakutupa huo uzima tusidhani kuwa hao walioenda Loliondo wamemkosea sana Mungu ndo maana leo wanapiga magoti kwa Babu they are humbled by grace na tukumbuke kuwa hujafa hujaumbika...Ni wangapi mnawapigia mafisadi magoti kwakuogopa vitumbua vyenu kuingia mchanga seuse uzima?
 
Namcheki Babu wa Loliondo kwenye taarifa ya habari TBC 1, na mmea huo wa utabibu wa magonjwa sugu unafanana na pareto.

Jamani sijui nijaribu kuchemsha maua ya pareto au sio wanajamvi?

kunywa pareto kwa afya yako....na pia ni kiburudisho
 
Eti babu kawekwa huko na edwaedi?? Nimesikia watu wakiteta kwenye kijiwe cha kahawa!
 
Eti babu kawekwa huko na edwaedi?? Nimesikia watu wakiteta kwenye kijiwe cha kahawa!

Edwaedi ni nani mkuu?

Hivi Watu wa kiingereza ni peeeeeeooopleeeeezzzz?

Naona shughuli za uchumi zimekuwa ghafla upande ule, wananchi wanalalamika kwenye TBC 1 kwamba nauli shs. 150,000/= kwa watu 8 kwenye kuruza. Au tuombe serikali ijenge barabara kwenda kwenye huo mgodi wa babu?
 
Mkuu.
Babu kapewa maono ya dawa hii na Mungu au Yesu?

Inaonekana Babu hakupewa amri au uono wa kuwa abague wagonjwa kulingana na imani zao za kidini.

Na Jee hao wagonjwa wamepewa sharti hilo la ku"kiri kuwa Yesu ni bwana"?

Hivi hapa Babu anafanya kazi ya uganga au uchungaji?
 
Tusishangae watu kwenda Loliondo. Mbona hatushangai watu wakifuata matibabu India, China na kwingineko?

Cha msingi tujadili kama watu wanapona ama la?
 
Kwa babu pamejaa sana nakuwa na wasiwasi kama huyu babu ataendelea kutoa dawa zaidi ya miezi miwili naimani loliondo itafahamika duniani kuliko tanzania na africa inavyojulikana duniani, kutakuwa na trip za ndege kutoka urop/asia/america to Loliondo kwa babu, tutegemee loliondo kuwa mji maarufu sana duniani
 


Mkuu kwa vile wewe ni mchungaji nisaidie kufahamu hivi vitu. na hayo yaliyopo post #20
 
kwani mtu ukichukua huo mti hautapona?i mean bila kumtumia babu

Kweli hata mimi najiuliza hili swali, maana nina mpango wa kuchukua mkopo benki nianzishe shamba kubwa la huu mti, nadhani italipa. Hapa kujiajiri nje nje.

Hata mimi nitauza kwa 500 tu kwa kijiko, yaani Euro aisee sio shilingi.
 
Preta naomba ukaninunulie spea za mbavu, yaani umevunja karibu zote, ila itabidi uagize orijino.

hihihihihi.....unataka spea za toyota au fiat?....mi naleta genuine kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…