Mambo ya mazoea ambayo yakageuka kuwa kama sheria

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
1. Chai na chapati mbili; yaani ukiwa mgahawani ukiagiza chai na chapati moja au zaidi ya mbili watu lazima wageuke kukuangalia, ni kama wamesikia wewe una ugonjwa wa corona bile.

2. Ukikaribishwa chakula sehemu ni lazima ukatae katae kidogo, wakikukazania kidogo ndipo unaenda kula; yaani ukaribishwe mara moja tu na uende kula! Hata aliyekukaribisha lazima ajiulize maswali, na kama alikukaribisha kwa kutania ni lazima ajutie kauli yake.

3. Mwanaume na mwanamke wanapolala kitanda kimoja, mwananamke lazima alale upande wa ukuta; yaani ikitokea mwanaume ukalala upande wa ukuta unajihisi kama umelala selo vile. Kwanza mwanaume unaanzaje kulala upande wa ukutani!??

4. Wali na maharage; binafsi huwa nikila wali ambao hauna maharage hua naona huo mchele umepotea bure kabisa.

5. Mgeni akija nyumbani akitaka kuvua viatu unamwambia haina haja ya kuvua viatu, aingie navyo tu. Najua wengi huwa hawamaanishi na kama wageni wakiingia na viatu ndani huwa wanaumia kimoyomoyo.

6.

7.
 
6.kupika ugali mchana, nyumba nyingi mchana lazima wapike ugali hata kama kuna chakula kingine

7.kupika wali usiku, nyumba nyingi usiku lazima upikwe wali maharage au wali nyama

8.chips na soda, karibu kila anayenunua chips lazima anunue na soda hasa coke ya baridi

9.kupiga mswaki na whitedent nyumba nyingi dawa ya meno wanayotumia ni whitedent

10.ukipikwa wali nyama,kila mtu achukue vipande vitatu tu vya nyamaπŸ˜‚ ukizidisha hapo unakomba mboga

11.kutazama taarifa ya habari saa mbili usiku, kuna watu mchana kutwa wapo tu hawafuatilii vyombo vya abari ila ikifika saa mbili ndio wanatazama habari, so breaking news hawazipati
 
Itakuwa mie ndio wa ajabu manake

1.Chai nakunywa na chapati moja
2.Nikikaribishwa chakula huwa sikatai,kama nikikataa huwa naenda moja kwa moja kwenye point either kilichopikwa huwa sili ama nimeshiba
4.Sipendi maharage
5.Mgeni akija kwetu akiingia na viatu fureshi,akitaka kuvua simkatazi
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
Kweli watnzania tunafahmiana vyema
Yaani mimi nikila wali mchana au ugali usiku naona kama tumbo haliko sawa kabisa.
 
Kweli wewe ni wa tofauti, chai chapati moja! Siku hizi nagonga tatu ila naona kama niongeze hadi nne au tano.
 
Write your reply...Guest lazima kuwe na ndala baba na mama au unakuta mguu wa kulia blue wa kushoto mwekundu na sabuni ndogo zile sjui zinaitwaje sjui give


kuku akichinjwa mpaka awe na kideri au sikukuu au kuna ugeni


boda boda piki piki mtaani kokote unapoenda buku mbili na ukiwa boda boda unajulikana muhuni pia ukikaa maskani vilevile


kupenda kuangalia season za kutafsiriwa haswa za kikorea uswahilini imekuwa kama sheria bila kusahau kuweka muziki kwenye flash kwenye vibanda


wavuta bangi kuhusishwa na uhuni mfano wizi


wakristo kufanya ibada jumapili tu na waislamu kwenda msikitini ijumaa tuuh
 
Aisee upo sawa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…